logo spc.r_ad0
sp.b_ad0
blu.strip
spc.bt_blu.strip
HABARI MPYA KITAIFA DAR MIKOANI TAHARIRI MAKALA MICHEZO
sp.b_menu
ban
sp.b_ban
jumapili, 10 septemba 2006
Pekua Tovuti
sp.t_sech.box sp.tafuta_w_tuma sp.t_tuma sp.r_tuma
sp.b_box sp.b_tuma
sp.b_F1
h.sep1
sp.r_men
sp.t
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari
sp.b_tuma
sp.l_men
h.sep1
sp.l sp.t sp.r
LOGIN
sp.men.l sp.men.t sp.men.r
Username
sp.b_user
sp.t-word
Password
sp.b_word
sp.t_btn
sp.b_btn
sp.b
h.sep1
tp.spc

Ligi ya vijana Ilala kuanza leo


na Joe Lwakatare

LIGI ya soka ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, inatarajiwa kuanza leo kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama cha Soka kwa Vijana Wadogo Wilaya ya Ilala (IDIYOSSA), Edwin Mloka ‘Father’, alisema kwamba maandalizi yamekamilika.

Alisema kwamba mchezo wa kwanza utafanyika saa 3:00 asubuhi, ambapo Manchester Kids itakipiga dhidi ya Msikate Tamaa, wakati mechi ya pili itawakutanisha Liwiti Kids dhidi ya Mdawa.

Mloka alisema kuwa mgeni rasmi katika michuano hiyo leo anatarajiwa kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Wilaya ya Ilala (IDFA), Mohammed Binda.

Mshindi wa kwanza katika michuano hiyo atazawadiwa seti moja ya jezi pamoja na sh 100,000 wakati mshindi wa pili atapata mipira miwili na mshindi wa tatu atapata mpira mmoja.

Timu nyingine zitakazoshiriki ligi hiyo ni Simba Kids, Dar Newala, Zalagoza, Mwiba Kids, Survivor Kids, Mogo Kids, River Heroes na DG Professionals.

 


h.sep

juu sp.b
Habari Mpya  |  Kitaifa  |  Dar  |  Mikoani  |  Tahariri  |  Makala  |  Michezo  |  Matangazo  |  Webmaster
Copyright 2006 © FreeMedia Ltd.
Free media limited
mtaa wa mkwepu na makunganya, slp 15261, dar es salaam, tanzania
simu +255-22-2120604  •  faksi +255-22-2126234