logo spc.r_ad0
sp.b_ad0
blu.strip
spc.bt_blu.strip
HABARI MPYA KITAIFA DAR MIKOANI TAHARIRI MAKALA MICHEZO
sp.b_menu
ban
sp.b_ban
jumatatu, 11 septemba 2006
Pekua Tovuti
sp.t_sech.box sp.tafuta_w_tuma sp.t_tuma sp.r_tuma
sp.b_box sp.b_tuma
sp.b_F1
h.sep1
sp.r_men
sp.t
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari
sp.b_tuma
sp.l_men
h.sep1
sp.l sp.t sp.r
LOGIN
sp.men.l sp.men.t sp.men.r
Username
sp.b_user
sp.t-word
Password
sp.b_word
sp.t_btn
sp.b_btn
sp.b
h.sep1
tp.spc

Faru mweusi aonekana Serengeti


Na Mwandishi Wetu, Serengeti

MMOJA wa wanyama aina ya faru weusi ambao ni adimu na wanaothaminika zaidi duniani, ameonekana ndani ya eneo lililo chini ya uongozi wa kampuni ya kitalii ya Grumeti Reserves Limited katika Wilaya ya Serengeti, mkoani Mara.

Habari za uhakika zilizopatikana jana wilayani hapa, zimesema mnyama huyo alianza kuonekana Ijumaa iliyopita katika eneo la Nyakitono linalopendekezwa kuwa Jumuiya ya Uhifadhi wa Wanyamapori (WMA) ambalo ni sehemu ya eneo linaloendeshwa na kampuni hiyo ya Kimarekani.

“Faru mweusi wa kike ambaye bado hajajulikana alikotoka, alionekana akichunga katika eneo la Nyakitono… hiyo ni neema kubwa kwetu, kwani wanyama wa aina hiyo ni adimu sana duniani,” alisema ofisa mmoja mwandamizi wa Kampuni ya Grumeti Reserves aliyetoa sharti la kutotajwa jina gazetini.

Kuonekana kwa mnyama huyo katika eneo hilo ni dalili nzuri za kuwahifadhi faru weusi 25 wanaotarajiwa kupelekwa siku chache zijazo ndani ya eneo linaloendeshwa na kampuni hiyo kwa kibali cha Serikali ya Tanzania.

Inaelezwa kuwa faru ni miongoni mwa wanyama ambao idadi yao imekuwa ikipungua kwa kasi kubwa duniani katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

 


h.sep

juu sp.b
Habari Mpya  |  Kitaifa  |  Dar  |  Mikoani  |  Tahariri  |  Makala  |  Michezo  |  Matangazo  |  Webmaster
Copyright 2006 © FreeMedia Ltd.
Free media limited
mtaa wa mkwepu na makunganya, slp 15261, dar es salaam, tanzania
simu +255-22-2120604  •  faksi +255-22-2126234