logo spc.r_ad0
sp.b_ad0
blu.strip
spc.bt_blu.strip
HABARI MPYA KITAIFA DAR MIKOANI TAHARIRI MAKALA MICHEZO
sp.b_menu
ban
sp.b_ban
jumatatu, 11 septemba 2006
Pekua Tovuti
sp.t_sech.box sp.tafuta_w_tuma sp.t_tuma sp.r_tuma
sp.b_box sp.b_tuma
sp.b_F1
h.sep1
sp.r_men
sp.t
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari
sp.b_tuma
sp.l_men
h.sep1
sp.l sp.t sp.r
LOGIN
sp.men.l sp.men.t sp.men.r
Username
sp.b_user
sp.t-word
Password
sp.b_word
sp.t_btn
sp.b_btn
sp.b
h.sep1
tp.spc

Maximo akunwa na chipukizi Stars


na Deodatus Mkuchu

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya Tanzania, ‘Taifa Stars’, Mbrazil Marcio Maximo, amekunwa na kiwango cha wachezaji chipukizi wa timu hiyo na kusema, wamempa shauku ya kuwapima wengine zaidi.

Maximo aliyetwaa mikoba ya timu hiyo Agosti 8, mwaka huu kutoka kwa Mzalendo, Dk. Mshindo Msolla, aliyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita wakati akizungumzia mechi iliyopita dhidi ya Burkina Faso na ijayo dhidi ya Msumbiji.

Alisema, wachezaji kama Henry Joseph na Athumani Iddi wa Simba, na Nizzar Khalfan wa Mtibwa Sugar ya Morogoro kwamba, licha ya ugeni wao katika kikosi hicho, wameonyesha uwezo mkubwa.

Maximo alisema, uwezo wa wachezaji hao umedhihirisha kwamba, soka si majina makubwa, hivyo ataendelea kuwapika chipukizi wengine kulingana na kiwango chao na si majina.

Kuhusu wachezaji kadhaa wanaotajwa kuwa wanafaa kuwamo katika kikosi hicho, Maximo alisema hamchukui mchezaji Stars kwa umaarufu wake bali kiwango.

Alisema, ipo siku Stars itakuwa na kiwango cha hali ya juu huku ikiwa haina wachezaji wenye majina makubwa, ingawa alisema, ni muhimu kwa timu ya taifa kuwa na wachezaji wanaocheza nje ya nchi.

Maximo alisema Stars isitarajie mteremko katika kundi lake, kwani kadiri inavyofanya vizuri, ndivyo inavyozidi kujijengea mazingira magumu kutokana na wapinzani kukaza buti tofauti na awali.

Akitoa mfano hai, Maximo alisema baada ya kufungwa na Senegal na kusikia Stars imeishinda Burkina Faso, Msumbiji imeamua kuwaita wachezaji wake wa kimataifa kukabiliana na Stars katika mechi ijayo.

 


h.sep

juu sp.b
Habari Mpya  |  Kitaifa  |  Dar  |  Mikoani  |  Tahariri  |  Makala  |  Michezo  |  Matangazo  |  Webmaster
Copyright 2006 © FreeMedia Ltd.
Free media limited
mtaa wa mkwepu na makunganya, slp 15261, dar es salaam, tanzania
simu +255-22-2120604  •  faksi +255-22-2126234