logo spc.r_ad0
sp.b_ad0
blu.strip
spc.bt_blu.strip
HABARI MPYA KITAIFA DAR MIKOANI TAHARIRI MAKALA MICHEZO
sp.b_menu
ban
sp.b_ban
jumanne, 12 septemba 2006
Pekua Tovuti
sp.t_sech.box sp.tafuta_w_tuma sp.t_tuma sp.r_tuma
sp.b_box sp.b_tuma
sp.b_F1
h.sep1
sp.r_men
sp.t
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari
sp.b_tuma
sp.l_men
h.sep1
sp.l sp.t sp.r
LOGIN
sp.men.l sp.men.t sp.men.r
Username
sp.b_user
sp.t-word
Password
sp.b_word
sp.t_btn
sp.b_btn
sp.b
h.sep1
tp.spc

ERB yaifuta Kampuni ya Linza


na Tamali Vullu

BODI ya Usajili ya Wakandarasi (ERB) imeifuta kampuni ya ujenzi ya Linza Concrete Designs kutoka kwenye orodha ya kampuni za ushauri za kihandisi.

Bodi hiyo pia imefuta jina la mkandarasi John Linza mwenye usajili namba CE 039 kutoka katika orodha ya wahandisi washauri.

Hayo yalielezwa jana na Mwenyekiti wa bodi hiyo, Profesa Burton Mwamila alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za bodi hiyo.

Alisema bodi imefikia uamuzi huo baada ya Mahakama Kuu kutupilia mbali pingamizi la mhandisi huyo kuhusu maamuzi ya bodi kumfuta katika bodi hiyo kutokana na kukiuka maadili ya taaluma hiyo.

“Kampuni ya Linza Concrete Designs pamoja na mkandarasi wake, Joseph Linza hawaruhusiwi kisheria kutoa huduma zozote za kiuhandisi tangu Novemba mwaka jana. Kwa hiyo wateja wote wanaotumia huduma za ushauri kutoka katika kampuni hii, wanaagizwa waache mara moja na wafuate huduma kutoka kwenye kampuni nyingine za uhandisi zilizosajiliwa.

“Bodi itaendelea kukagua maeneo yote ya ujenzi yaliyokuwa chini ya uangalizi wa kampuni hiyo ambayo inafanya kazi katika ‘site’ zaidi ya 50, ili kuhakikisha kwamba sheria hii inafuatwa,” alisema mwenyekiti huyo.

Aliyataja baadhi ya majengo yanayojengwa na kampuni hiyo kuwa ni Plot 24 Block 56 lililopo Sikukuu/Narung’ombe, Plot 23 Block 48 Sikukuu/Mafia, Plot 12 Block 34 Swahili/Mafia, Plot 29 Swahili/Mchikichini, Plot 107 Block E Muhonda/Muheza, Plot 24 Block A Uhuru/Ndanda, Plot 13 Block J Congo/Mafia na Plot 3 Block 21 Mtaa wa Lindi.

Alisema kuwa Septemba 23, mwaka 2004, bodi ilitembelea maeneo ambayo kampuni hiyo inafanyia shughuli zake na kubaini ukiukwaji wa taaluma ya uhandisi.

Profesa Mwamila alisema kampuni hiyo ilipewa miezi mitatu kurekebisha kasoro hizo, lakini baada muda huo ilikuwa haijarekebisha kasoro hizo, hivyo bodi ilichukua uamuzi wa kuifuta.

Alisema Novemba 7, mwaka jana, kampuni hiyo, ilipinga uamuzi huo kwa kufungua kesi katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, lakini Julai 21, mwaka huu Mahakama Kuu ilitupilia mbali pingamizi hilo, hivyo uamuzi wa bodi uko palepale.

 


h.sep

juu sp.b
Habari Mpya  |  Kitaifa  |  Dar  |  Mikoani  |  Tahariri  |  Makala  |  Michezo  |  Matangazo  |  Webmaster
Copyright 2006 © FreeMedia Ltd.
Free media limited
mtaa wa mkwepu na makunganya, slp 15261, dar es salaam, tanzania
simu +255-22-2120604  •  faksi +255-22-2126234