VIGOGO mjini hapa ndio wanaoongoza kwa kuiibia maji Mamlaka ya Majisafi na Majitaka mjini Dodoma (DUWASA).
Hayo yamebainishwa juzi mjini hapa na Mkurugenzi wa mamlaka hiyo, Peter Mokiwa, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Alisema wafanyabiashara maarufu, wamiliki wa hoteli na vigogo serikalini ndio wanaoongoza kuiibia mamlaka hiyo kwa kujiunganishia maji kinyume cha sheria, jambo ambalo limekuwa likiiingizia mamlaka hiyo hasara kubwa.
Alisema kutokana na wizi huo, mamlaka hiyo imepata hasara ya sh milioni 53 katika kipindi cha kuanzia Januari 2005 hadi Juni 2006.
“Wamiliki wa hoteli, vigogo wanaofanya kazi serikalini na wafanyabiashara maarufu ndio wanaoongoza kwa kuiba maji na wanapokamatwa wanapatwa na shinikizo la damu na kuzirai,” alisema Mokiwa.
Pia mkurugenzi huyo alisema kutokana na watu hao kuambiwa wanatakiwa kulipa kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya faini ya kujiunganishia maji kinyume cha sheria, alisema sasa wameanzisha huduma ya kwanza kwa kuwa vigogo hao wamekuwa wakizirai baada ya kupewa taarifa ya kulipa fedha nyingi.
Mokiwa alisema watu wa kawaida ndio wanaoongoza kwa kulipa ankara za maji bila matatizo yoyote ikilinganishwa na watu wenye uwezo ambao hudhani kuwa kutokana na wadhifa walionao hawawezi kuchukuliwa hatua za kisheria