logo spc.r_ad0
sp.b_ad0
blu.strip
spc.bt_blu.strip
HABARI MPYA KITAIFA DAR MIKOANI TAHARIRI MAKALA MICHEZO
sp.b_menu
ban
sp.b_ban
jumanne, 12 septemba 2006
Pekua Tovuti
sp.t_sech.box sp.tafuta_w_tuma sp.t_tuma sp.r_tuma
sp.b_box sp.b_tuma
sp.b_F1
h.sep1
sp.r_men
sp.t
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari
sp.b_tuma
sp.l_men
h.sep1
sp.l sp.t sp.r
LOGIN
sp.men.l sp.men.t sp.men.r
Username
sp.b_user
sp.t-word
Password
sp.b_word
sp.t_btn
sp.b_btn
sp.b
h.sep1
tp.spc

Wachanga ng’ombe kujenga sekondari


na David Frank, Arusha

WAKAZI wa Kata ya Sepeko wilayani Monduli, wamechanga ng'ombe zaidi ya 200 ili kusaidia ujenzi wa shule ya sekondari katika kata hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano wa kuhamasisha mchango huo katika Kijiji cha Mti Mmoja juzi, diwani wa kata hiyo, Loota Sanare alisema ng'ombe hao wamechangwa na wananchi wa vijiji vinane vya kata hiyo.

Alisema hivi sasa bado michango inaendelea katika kata hiyo na lengo ni kukusanya sh zaidi ya milioni 400 ambazo zitaweza kukamilisha sekondari hiyo.

Sanare alisema kutokana na makubaliano waliyofikia, kila kijiji kimekubali kuchangia ujenzi wa madarasa mawili na nyumba za walimu na kulingana na uwezo, vijiji vingine vimekubali kujenga ofisi.

Alisema vijiji ambavyo vinachangia ujenzi huo ni pamoja na Alkaria, Alkatan, Repolko, Losimongori, Lashaine, Lendikinya, Meserani Juu na Mti Mmoja.

Diwani huyo alisema sekondari hiyo, inatarajiwa kujengwa katika Kijiji cha Mti Mmoja na itajulikana kama Nanja Sekondari na itaanza na wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne.

 


h.sep

juu sp.b
Habari Mpya  |  Kitaifa  |  Dar  |  Mikoani  |  Tahariri  |  Makala  |  Michezo  |  Matangazo  |  Webmaster
Copyright 2006 © FreeMedia Ltd.
Free media limited
mtaa wa mkwepu na makunganya, slp 15261, dar es salaam, tanzania
simu +255-22-2120604  •  faksi +255-22-2126234