logo spc.r_ad0
sp.b_ad0
blu.strip
spc.bt_blu.strip
HABARI MPYA KITAIFA DAR MIKOANI TAHARIRI MAKALA MICHEZO
sp.b_menu
ban
sp.b_ban
jumanne, 12 septemba 2006
Pekua Tovuti
sp.t_sech.box sp.tafuta_w_tuma sp.t_tuma sp.r_tuma
sp.b_box sp.b_tuma
sp.b_F1
h.sep1
sp.r_men
sp.t
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari
sp.b_tuma
sp.l_men
h.sep1
sp.l sp.t sp.r
LOGIN
sp.men.l sp.men.t sp.men.r
Username
sp.b_user
sp.t-word
Password
sp.b_word
sp.t_btn
sp.b_btn
sp.b
h.sep1
tp.spc

Pazia kufunguliwa leo
LIGI YA MABINGWA ULAYA...


LONDON, England

HAINA shaka kwamba unakumbuka kilichotokea Mei 17, mwaka huu pale Barcelona ilipoigeuzia kibao Arsenal katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Fainali hiyo ilikuwa gumzo pengine kuliko miaka yote. Ilifanyika Uwanja wa Stade de France, uliopo Saint Dennis, nje kidogo ya Jiji la Paris, kaskazini mwa Ufaransa.

Ikumbukwe tu kwamba uwanja huo uliwahi kuwaliza Brazil katika fainali ya Kombe la Dunia mwaka 1998 ambako wenyeji Ufaransa walishinda mabao 3-0.

Uhondo wa michuano hii yenye mvuto na utajiri mkubwa wa fedha katika ngazi za klabu duniani, unatarajiwa kuanza tena leo katika viwanja vinane tofauti kumsaka bingwa wa msimu wa 2006/7.

Je, kuna wa kumvua taji Barcelona? Bila shaka hilo ni swali wanalojiuliza wadau wa soka kutokana na ubora wa timu hiyo.

Lakini mshambuliaji na Mwanasoka Bora wa Dunia, Ronaldo de Meraira maarufu kama Ronaldinho Gaucho, anatamba kwamba Barcelona itatetea taji hilo.

“Tutapenda kuthibitisha hilo kwa kuisulubu Chelsea. Ni timu nyepesi, naamini hata wengine tutakutana nao kwa lengo la kukamilisha ratiba, lakini siamini kama kuna timu ya kutuzuia,” anasema.

Jeuri ya Ronaldinho inatokana na kuwa na safu imara ya ushambuliaji yenye nyota kama Samuel Eto’o Fils, mkali asiyekaukiwa mabao. Pia wamo Eidur Gudjohnsen aliyesajiliwa msimu huu kutoka Chelsea, Javier Saviola, Santiago Ezquerro na Oriol Riera katika ushambuliaji. Safu yake ya ulinzi ina nguvu ya ziada ya kina Gianluca Zambrotta na Lilian Thuram waliotua kutoka Juventus ya Italia.

Barcelona itatupa karata ya kwanza ya kampeni za kutetea taji kwa kuumana na Levski Sofia ya Bulgaria kwenye Uwanja wa Nou Camp, jijini Barcelona Hispania leo kuanzia saa 3:45 usiku.

Mbali ya mchezo huo, michezo mingine ya leo, Bayern Munich ya Ujerumani itapepetana na Spartak Moscow ya Urusi, huku Chelsea wakiwakaribisha Werder Bremen kutoka Ujerumani.

Jose Mourinho, Kocha wa Chelsea, amejaza nyota baada ya kuwanyakua Andriy Shevchenko, Ashley Cole, Salomon Kalou, Michael Ballack na John Obi Mikel ili waweze kushirikiana na kina Frank Lampard, John Terry, Didier Drogba na wengine.

Anaamini kwamba, licha ya kuwa na kampeni za kutetea ubingwa wa England, kazi kubwa aliyonayo ni kuipa klabu yake ubingwa wa Ulaya kwa mara ya kwanza.

“Inawezekana. Kikosi hiki kina jeuri ya kupiga ndani na nje, kwa maana ya England na nje ya England. Tusubiri, lakini dhamira ya Chelsea ni kufanya kweli mwaka huu,” anasema Mourinho aliyeipa ubingwa wa Ulaya FC Porto ya Ureno msimu wa 2004/5.

Nao watemi wa mwaka 2005/6, Liverpool ya England wanaanzia ugenini Uholanzi dhidi ya PSV iliyoongeza nguvu ya mshambuliaji tishio kwa mipira ya kichwa, Patrick Kluivert.

AS Roma ya Italia iliyokimbiwa na nyota wake kama Nonda Shabani na Samuel Kuffour, itaanzia kazi kwa Shakhtar Donetsk ya Ukraine, Galatasaray ya Uturuki itachuana na Bordeaux ya Ufaransa, wakati Olympiakos ya Ugiriki itakuwa nyumbani kukipiga na Valencia ya Hispania. Sporting Lisbon ya Ureno iko nyumbani Lisbon ikinoa makali kabla ya kuwavaa Inter Milan ya Italia. Ngoma zote zitaanza kupigwa leo saa 3:45 usiku.

Mara baada ya kazi pevu ya leo, kesho, Arsenal walionyang’anywa tonge mdomoni na Barcelona iliyoshinda 2-1 katika mchezo wa fainali Mei mwaka huu, ikiwa na nyota wake katika upachikaji wa mabao, Thierry Henry, imepania kurudi katika fainali na kwamba itachomoa makucha yake kuanzia kesho dhidi ya Hamburg ya Ujerumani.

Kocha Arsene Wenger wa Arsenal anasema kwamba, licha ya kuanzia ugenini, amepania kuvuna pointi tatu.

Wakali wengine wa England, Manchester United wanaofundwa na Sir Alex Ferguson, kwa miaka 21 sasa, wako nyumbani Uwanja wa Old Trafford kujaribu ngekewa yao mbele ya jirani zao Celtic ya Uskochi.

AC Milan ya Italia itaikaribisha AEK Athens ya Ugiriki, huku Anderlecht ya Ubelgiji ikiwa mwenyeji wa Lille ya Ufaransa. Dinamo Kiev ya Ukraine itacheza na Steaua Buccuresti ya Romania.

Lakini ngoma nzito itakuwa kati ya Olympique Lyon ya Ufaransa, timu ngumu isiyo na kelele nje ya uwanja, dhidi ya Real Madrid, wakali wenye mkusanyiko wa nyota halisi wa soka kutoka kona zote za dunia.

Unatarajiwa kuwa mtihani mgumu kwa Real Madrid kutokana na kucheza ugenini, lakini Kocha Fabio Capello anasema amekuja Hispania kwa lengo la kurudisha heshima ya Real Madrid katika ligi na michuano ya kimataifa. Michezo mingine kesho ni kati ya FC Copenhagen ya Denmark na Benfica ya Ureno, huku FC Porto ya Ureno ikionyeshana kazi na CSKA Moscow ya Urusi.

Je, wakati mambo yanaanza rasmi leo, ni nani atakuwa na makali ya kuivua taji Barcelona msimu huu? Bila shaka ni jambo la kusubiri na kuona baada ya miezi minane.

 


h.sep

juu sp.b
Habari Mpya  |  Kitaifa  |  Dar  |  Mikoani  |  Tahariri  |  Makala  |  Michezo  |  Matangazo  |  Webmaster
Copyright 2006 © FreeMedia Ltd.
Free media limited
mtaa wa mkwepu na makunganya, slp 15261, dar es salaam, tanzania
simu +255-22-2120604  •  faksi +255-22-2126234