logo spc.r_ad0
sp.b_ad0
blu.strip
spc.bt_blu.strip
HABARI MPYA KITAIFA DAR MIKOANI TAHARIRI MAKALA MICHEZO
sp.b_menu
ban
sp.b_ban
jumanne, 26 septemba 2006
Pekua Tovuti
sp.t_sech.box sp.tafuta_w_tuma sp.t_tuma sp.r_tuma
sp.b_box sp.b_tuma
sp.b_F1
h.sep1
sp.r_men
sp.t
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari
sp.b_tuma
sp.l_men
h.sep1
sp.l sp.t sp.r
LOGIN
sp.men.l sp.men.t sp.men.r
Username
sp.b_user
sp.t-word
Password
sp.b_word
sp.t_btn
sp.b_btn
sp.b
h.sep1
tp.spc

Makamu wa Museveni aeleza alivyonusurika Thailand

l_pic0
Profesa Gilbert Bukenya


KAKIRI, Uganda

MAKAMU wa Rais, Profesa Gilbert Bukenya, ameeleza jinsi alivyoweza kurudi nyumbani salama kutoka Bangkok, Thailand, ambako kulitokea mapinduzi ya kijeshi.

Bukenya aliyeonekana mchangamfu aliliambia Gazeti la Daily Monitor nyumbani kwake huko Kakiri, Ijumaa iliyopita kwamba alilindwa vyema wakati serikali ya nchi hiyo ilipoangushwa.

“Nililindwa kwa kikosi chenye magari ya Mercedes Benz yapatayo sita na walinzi 27 nikiwa kwenye hoteli niliyofikia,” Bukenya alisema.

“Baadhi yao walikuwa askari polisi, wengine walikuwa makachero wa upelelezi na wengine kutoka jeshini. Lakini nilivyosoma magazeti asubuhi hii (Ijumaa), watu walikuwa wakisema kwamba Bukenya amekwama kwenye chumba cha hoteli. Kivipi?” alihoji.

Wakati Daily Monitor lilipomtembelea Bukenya kwenye makazi yake, alivaa ukakamavu wa kijeshi na alikutwa akiwahutubia wakazi wa Busiro Kaskazini ambayo ni sehemu ya jimbo lake, juu ya mbinu mpya za kubuni njia za kujijengea utajiri kwa njia ya ulimaji wa mpunga, mahindi na maharage.

Wiki iliyopita, Bukenya alijikuta katika wakati mgumu muda mfupi baada ya mapinduzi wakati alipoalikwa kwa chakula cha usiku na aliyekuwa Naibu Waziri Mkuu Chidchai Vanasatidya, kwenye Ikulu ya nchi hiyo. Siku iliyofuata Ikulu iliangukia mikononi mwa wapangaji wa mapinduzi hayo waliofanikiwa kumuangusha Waziri Mkuu Thaksin Shinawatra, kutoka madarakani huku Vanasatidya akitiwa mbaroni.

Lakini wakati habari za mapinduzi zilipoibuka, Profesa Bukenya alikuwa akifurahia maisha, kwa mujibu wa katibu wake wa habari.

Pia alitembelea Taassisi ya Kilimo cha Mpunga ya Thailand na Kampuni ya Sor Heng Noodle.

“Wakati makamu wa rais alipofanikiwa kurudi hotelini kwake, hakukuwa na matatizo yoyote kwani alienda kufanya mazoezi ‘gym’. Na alikuwa akifurahia maisha hotelini kabla ya kuibuka kwa habari za mapinduzi,” Katibu huyo Linda Nabusayi, alisema katika taarifa yake juzi.

“Nyakati za asubuhi, hakukuwa na dalili za mapinduzi mitaani na shughuli za kila siku ziliendelea kama kawaida. Habari pekee tulizoletewa na wenyeji wetu zilisema: “Kutokana na matukio yaliyotokea usiku wa jana, tunashika madaraka ya shughuli za kiserikali na balozi zote zimeshauriwa kwa mwenendo mzima wa leo. Leo imetangazwa siku ya mapumziko kitaifa na shughuli zote za kibiashara, shule, mabenki na ofisi za serikali zimefungwa.”

Hata hivyo, Bukenya alisema kwamba alishtushwa na kuingiwa na hofu na habari za kuangushwa kwa wenyeji wake lakini alipata imani wakati mkuu wa usalama wake aliyemhakikishia kwamba hakuna haja ya kushtuka kwani kila kitu kipo mahali pake.

Pamoja na kuhakikishiwa usalama hata hivyo aliambiwa asitoke hotelini pamoja na kwamba alihakikishiwa kwamba programu yake ya kutembelea maeneo mbalimbali haitaingiliwa. Bukenya alisema kwamba alifanya mikutano na wafanyabiashara maarufu wa Thailand waliosema kwamba watakubaliana na serikali mpya.

MONITOR


h.sep

juu sp.b
Habari Mpya  |  Kitaifa  |  Dar  |  Mikoani  |  Tahariri  |  Makala  |  Michezo  |  Matangazo  |  Webmaster
Copyright 2006 © FreeMedia Ltd.
Free media limited
mtaa wa mkwepu na makunganya, slp 15261, dar es salaam, tanzania
simu +255-22-2120604  •  faksi +255-22-2126234