logo spc.r_ad0
sp.b_ad0
blu.strip
spc.bt_blu.strip
HABARI MPYA KITAIFA DAR MIKOANI TAHARIRI MAKALA MICHEZO
sp.b_menu
ban
sp.b_ban
jumamosi, 10 Novemba 2007
Pekua Tovuti
sp.t_sech.box sp.tafuta_w_tuma sp.t_tuma sp.r_tuma
sp.b_box sp.b_tuma
sp.b_F1
h.sep1
sp.r_men
sp.t
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari
sp.b_tuma
sp.l_men
h.sep1
sp.l sp.t sp.r
LOGIN
sp.men.l sp.men.t sp.men.r
Username
sp.b_user
sp.t-word
Password
sp.b_word
sp.t_btn
sp.b_btn
sp.b
h.sep1
tp.spc


Umeme wa uhakika Kigoma Des. 2009
MBUNGE JIMBO LA KIGOMA MJINI


na Irene Mark na Rahel Chizoza, Dodoma


WAZIRI wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, amesema baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Kigoma, yatapata umeme wa uhakika Desemba 2009.

Alisema kuchelewa kwa mpango wa serikali kufikisha umeme mkoani humo kunatokana na taratibu ndefu za uagizaji wa mashine mpya ya kuzalisha umeme kutoka nje.

Karamagi alilazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya swali la nyongeza la Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba (CCM), aliyetaka kufahamu sababu za ahadi ya Rais Jakaya Kikwete ya kufikisha umeme katika mkoa huo kusogezwa.

“Nataka kufahamu…wakati Rais Kikwete alipotembelea Kigoma aliahidi kuwa tutapata umeme Januari 2009, leo naibu waziri anasema tutapata umeme huo Desemba 2009, kwa nini mnachelewa?

“Wakati wenzetu wanazungumzia kupeleka umeme vijijini sisi tunatarajia kuona umeme kwenye ofisi ya makao makuu ya mkoa...hivi ni lini Kigoma tutapata huduma hii kwa uhakika?” alihoji Serukamba kwa masikitiko.

Katika majibu yake, Karamagi alisema ili kuondoa upungufu wa umeme mkoani Kigoma, serikali imeagiza mashine mpya yenye uwezo wa kuzalisha kilowati 2,000 na kwamba makubaliano kati ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na Kampuni ya Anglo Belgium Corporation yamekamilika na unatarajia kuingia nchini Desemba 2009.

Katika swali la msingi, Serukamba alitaka kufahamishwa hatua zilizofikiwa za utekelezaji wa mpango wa kuupatia Mkoa wa Kigoma umeme wa uhakika na mkakati wa kuweka umeme wa dharura wakati ukisubiriwa muda wa utekelezaji wa mpango wa awali.

Aidha, Waziri Karamagi alibainisha kuwa katika kipindi cha mwaka 2008 hadi 2012, serikali itajenga kituo cha kuzalisha umeme wa maji kwenye Mto Malagarasi kitakachotoa kilowati 8,000. Mradi huo utafadhiliwa na Millenium Challenge Corporation (MCC) la Marekani.



h.sep

juu sp.b
Habari Mpya  |  Kitaifa  |  Dar  |  Mikoani  |  Tahariri  |  Makala  |  Michezo  |  Matangazo  |  Webmaster
Copyright 2007 © FreeMedia Ltd.
Free media limited
mtaa wa Mkwepu na Makunganya, jengo la Bilicanas, gorofa ya kwanza, SLP 15261, Dar es salaam, Tanzania
simu +255-22-2126233  •  faksi +255-22-2126234  •  Selula  0713 296570