logo spc.r_ad0
sp.b_ad0
blu.strip
spc.bt_blu.strip
HABARI MPYA KITAIFA DAR MIKOANI TAHARIRI MAKALA MICHEZO
sp.b_menu
ban
sp.b_ban
jumamosi, 10 Novemba 2007
Pekua Tovuti
sp.t_sech.box sp.tafuta_w_tuma sp.t_tuma sp.r_tuma
sp.b_box sp.b_tuma
sp.b_F1
h.sep1
sp.r_men
sp.t
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari
sp.b_tuma
sp.l_men
h.sep1
sp.l sp.t sp.r
LOGIN
sp.men.l sp.men.t sp.men.r
Username
sp.b_user
sp.t-word
Password
sp.b_word
sp.t_btn
sp.b_btn
sp.b
h.sep1


Polisi hana haki ya kumpiga mtuhumiwa!
Mohamed Majaliwa


NI hali ya kawaida unapouliza swali kwa mtu yeyote hasa kijana, na jibu lake likawa ni ‘unauliza makofi polisi?’

Jibu hili humaanisha kwamba swali ulilouliza jibu lake lipo wazi na hakutegemea kama hilo lingekuwa ni swali kwako.

Kauli hii imezoeleka kutokana na ukweli kwamba, kipigo toka kwa polisi hasa kwa mtuhumiwa, ni jambo la kawaida sana ambalo halipaswi kuulizwa.

Hii hutokea pindi mtuhumiwa afikishwapo mikononi mwa polisi hasa wa vituoni ambako hupokewa kwa makofi na mabuti yasiyo idadi.

Kuna msemo wa Waswahili usemao kuwa, ‘kawaida ni kama sheria’, na hii ni kawaida ambayo miongoni mwa askari polisi wengi imekuwa ni kama utaratibu wa kisheria kumpokea mtuhumiwa kwa kipigo.

Kipigo pia imekuwa ni kawaida wakati wa mahojiano kati ya polisi na mtuhumiwa ambako hulenga kumlazimisha kutoa au kukubali maelezo fulani ambayo hutumika kama ushahidi mahakamani.

Sasa basi, kutokana na kutokujua sheria na haki zao kwa ujumla kama watuhumiwa, raia wengi wapatao dhahma hii, wamekuwa wakipuuza na kuiacha iendelee bila kujua kuwa ni ukiukwaji wa haki na uvunjaji wa sheria.

Kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai, pamoja na haki nyingine nyingi, mtuhumiwa pia ana haki ya kuheshimiwa na kusikilizwa. Hii imekuwa tofauti na mwenendo wa kipolisi zaidi ya mtuhumiwa ambapo mtuhumiwa huchukuliwa kama mtu asiye na thamani yoyote mbele ya askari polisi.

Kitendo cha polisi hasa katika vituo mbalimbali vya polisi kuwa na desturi ya kutoa kipigo kwa mtuhumiwa, hasa wakati anapofikishwa katika mikono yao na wakati wa kuchukua maelezo ya awali ambayo hutumika kama ushahidi mahakamani, kunakiuka maelekezo na matakwa ya sheria ya ushahidi.

Sheria hii pamoja na mambo mengine, inaeleza masharti ya kupokelewa kwa ushahidi mbele ya mahakama wakati wa usikilizaji mashauri ya jinai.

Inaeleza kuwa aina yoyote ya ushahidi utolewao mahakamani, ni sharti uwe umetolewa kwa uhuru na hiyari ya dhati ya mtoaji, yaani pasipo kushurutishwa na mtu mwingine kwa namna yoyote.

Hivyo kwa kumpiga mtuhumiwa wakati wa utoaji wa maelezo, ni kupunguza uhuru wa mtuhumiwa katika utoaji huo wa maelezo au ushahidi.

Na endapo itathibitishwa mbele ya mahakama kuwa maelezo ya awali ya mtuhumiwa yamepatikana kwa njia ya kipigo au vitisho vya aina yoyote, maelezo hayo ni batili na hivyo hayatakubaliwa na mahakama kama ushahidi kwa kesi husika.

Na ikumbukwe kuwa endapo itatokea mahakama itaruhusu ushahidi huo kutumika katika kesi husika bila kuzingatia pingamizi kuwa ushahidi huo ulipatikana kwa njia ya kipigo na vitisho, basi inaweza kuwa ni sababu nzuri ya mtuhumiwa kukata rufaa zidi ya hukumu iliyotolewa zaidi yake ambayo maamuzi yake yamefikiwa kwa kutumia ushahidi huo batili.

Ikumbukwe kuwa ushahidi ndio msingi wa kesi yoyote katika kufikia maamuzi sahihi na ya haki, hivyo msingi wa hukumu ukikosekana, hukumu hiyo inaweza kuangushwa wakati wowote kwa njia ya rufaa.

Kwa kumpokea mtuhumiwa kwa kipigo na vitisho, polisi pia wanakuwa wanakiuka misingi ya haki za asili, yaani “Natural justice’.

Moja ya misingi hii inaeleza kuwa, mtuhumiwa hatochukuliwa kama mkosaji au mhalifu, mpaka pale ambapo itathibitishwa na sheria kuwa ni mkosaji.

Hii inajulikana kitaalamu kama ‘Presumption of Innocent until proved guilty’. Hivyo basi, kitendo cha polisi kuanza kumpokea mtuhumiwa kwa makofi na adhabu nyingine, ni kumuadhibu mtuhumiwa kabla ya hukumu ya kisheria kupitishwa na chombo chenye mamlaka ya kufanya hivyo ambacho ni mahakama.

Zaidi, pia kitendo hiki kinakinzana na sheria, hasa kutokana na ukweli kuwa, hukumu inaweza kuamua kuwa kutokana na ushahidi uliowasilishwa mahakamani, imeonekana kuwa mtuhumiwa si mkosaji, yaani hana hana kesi ya kujibu na hivyo kumuachia huru mbali na kutomtia hatiani.

Hivyo kwa kumuadhibu mtuhumiwa kabla ya hukumu, itamaanisha kumsababishia adhabu ambayo hakustahili.

Na ikumbukwe kuwa, endapo ushahidi uliopo mbele ya mahakama tayari kwa kutumika katika kesi husika ulipatikana katika mazingira niliyoeleza awali, basi ni jukumu la mtuhumiwa au wakili wake kuiambia mahakama kuwa ushahidi huo ni batili kutokana na mazingira ya upatikanaji wake.

 
Simu: 0786 809798
Barua pepe: almajah2000@yahoo.com

 


h.sep
juu sp.b
Habari Mpya  |  Kitaifa  |  Dar  |  Mikoani  |  Tahariri  |  Makala  |  Michezo  |  Matangazo  |  Webmaster
Copyright 2007 © FreeMedia Ltd.
Free media limited
mtaa wa Mkwepu na Makunganya, jengo la Bilicanas, gorofa ya kwanza, SLP 15261, Dar es salaam, Tanzania
simu +255-22-2126233  •  faksi +255-22-2126234  •  Selula  0713 296570