logo spc.r_ad0
sp.b_ad0
blu.strip
spc.bt_blu.strip
HABARI MPYA KITAIFA DAR MIKOANI TAHARIRI MAKALA MICHEZO
sp.b_menu
ban
sp.b_ban
jumapili, 11 Novemba 2007
Pekua Tovuti
sp.t_sech.box sp.tafuta_w_tuma sp.t_tuma sp.r_tuma
sp.b_box sp.b_tuma
sp.b_F1
h.sep1
sp.r_men
sp.t
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari
sp.b_tuma
sp.l_men
h.sep1
sp.l sp.t sp.r
LOGIN
sp.men.l sp.men.t sp.men.r
Username
sp.b_user
sp.t-word
Password
sp.b_word
sp.t_btn
sp.b_btn
sp.b
h.sep1
tp.spc


Wafikishwa mahakamani kwa kutupa mwili wa marehemu


na Patrick Mabula, Kahama


WAKAZI wawili wa mjini hapa wameshitakiwa mahakamani kwa kosa la kutupa porini maiti ya mtu aliyekufa akiwa nyumbani kwa mganga wa kienyeji.

Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Inspekta Said Gingo, alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya, Juma Hassan kuwa washitakiwa walitenda kosa hilo Oktoba, 29 katika Kijiji cha Bunegezi, Bukombe mkoani Shinyanga.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Mathias Hengeli (50) na Punja gwanzila (17), wote wakazi wa Kijiji cha Bunegezi, Shinyanga ambao walikuwa wakiishi nyumbani kwa mganga huyo kama wasaidizi wake.

Gingo aliendelea kueleza mahakamani kuwa washitakiwa walimtupa marehemu, Kasamwa Shilagila, aliyekuwa akitibiwa nyumbani kwa mganga huyo baada kufariki.

Alidai kuwa mganga huyo alitoroka baada ya kuona mgonjwa wake kafariki na wasaidizi wake waliamua kuuchukua mwili wa marehemu kwenda kuutupa porini ili kuondoa usumbufu wa kuulizwa na ndugu zake waliokuwa wakifika kumjulia hali nyumbani kwa mganga huyo.

Gingo alidai kuwa mwili wa marehemu uliokotwa na wasamaria wema ukiwa umeharibika lakini ndugu zake walifanikiwa kuutambua.

Washitakiwa walikamatwa baada ya kugundulika kuwa wasaidizi wa mganga na kupatikana taarifa za awali kuwa ndio walioubeba mwili huo kwenda kuutupa porini.

Washitakiwa walirudishwa rumande hadi Novemba 20 kesi yao itakapotajwa tena, na polisi wanaendelea kumsaka mganga wa jadi aliyekimbia.


h.sep

juu sp.b
Habari Mpya  |  Kitaifa  |  Dar  |  Mikoani  |  Tahariri  |  Makala  |  Michezo  |  Matangazo  |  Webmaster
Copyright 2007 © FreeMedia Ltd.
Free media limited
mtaa wa Mkwepu na Makunganya, jengo la Bilicanas, gorofa ya kwanza, SLP 15261, Dar es salaam, Tanzania
simu +255-22-2126233  •  faksi +255-22-2126234  •  Selula  0713 296570