logo spc.r_ad0
sp.b_ad0
blu.strip
spc.bt_blu.strip
HABARI MPYA KITAIFA DAR MIKOANI TAHARIRI MAKALA MICHEZO
sp.b_menu
ban
sp.b_ban
jumapili, 16 Desemba 2007
Pekua Tovuti
sp.t_sech.box sp.tafuta_w_tuma sp.t_tuma sp.r_tuma
sp.b_box sp.b_tuma
sp.b_F1
h.sep1
sp.r_men
sp.t
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari
sp.b_tuma
sp.l_men
h.sep1
sp.l sp.t sp.r
LOGIN
sp.men.l sp.men.t sp.men.r
Username
sp.b_user
sp.t-word
Password
sp.b_word
sp.t_btn
sp.b_btn
sp.b
h.sep1


Kauli za wananchi kuhusu huduma zinazotolewa na TRL
Wasemavyo Wasomaji


Suala la kumpata mwekezaji kwa shirika hilo halina faida kwa Watanzania, mpaka sasa hakuna kipya, mabehewa na reli ni vile vile. Hali hairidhishi kwa ujumla. Walter Thomas - Hai, Moshi. 0753-943000.

Huyu mwekezaji mpya wa TRC ni mbambashaji, huduma ya usafiri wa treni bado mbaya. Wananchi hasa wa Kigoma bado wanateseka. Serikali imechemsha. E.R Chomola - Tanga. 0784-635209.

Huduma si mbaya tatizo lipo kwa watekelezaji, viongozi wanapaswa kujua kosa lipo wapi, isije kuwa kanzu mpya sheikh yule yule. Mdimi Moody - Mtaa wa Rufiji, Mwanza. 0756- 355594.

Kulingana na malalamiko kutoka kwa wasafiri, TRL imeshindwa kuboresha huduma hiyo. Waziri mwenye dhamana angalia hao ving'ang'anizi wachache watakuharibia kwa masilahi yao. 0786-474267.

Huduma za TRL haziridhishi hata kidogo, kwa maoni yangu mwekezaji aache kutoa huduma hiyo kwa sababu imekuwa adha kubwa kwa wananchi, hakuna lolote jipya. Peter, Dar es Salaam. 0787-060846.

Hakuna jipya watakalofanya hao wawekezaji wapya wa TRL, mimi nadhani ni ubakaji wa uchumi, wakishapata wanachotaka wanaishia zao kama ilivyokuwa kwa ATC. 0713-211065.

Kwa maoni yangu, serikali inapaswa ikae chini na kutafakari hizi huduma zinazotolewa na huyu mwekezaji kama ndizo zilizokusudiwa. Inatuwia vigumu sisi wasafiri tunaotumia njia hii kuamini kama huyu ndiye mwekezaji aliyekuja kuboresha huduma za usafiri wa reli. Ramadhani M, Mara. 0782-189176.

Usafiri wa treni ni mbaya sana kuliko ilivyokuwa miaka ya 88 hadi 90. Watu wanajazwa kwenye mabehewa kupita kiasi, mabehewa ni mabovu, huduma kwa ujumla ni mbovu. Serikali inapaswa kulimulika hili, isisubiri mpaka ajali ya kupoteza maisha ya maelfu ya watu ndipo ichukue hatua. 0713-497339.

Huduma zinazotolewa na TRL ni mbovu, safari zimepungwa kwa asilimia hamsini, mabehewa machafu, ratiba haifuatwi, huduma ya chakula ipo chini ya kiwango cha ubora, bei ni kubwa. Hakuna maboresha kwa huduma hii bali kuwadhalilisha wasafiri wa Kanda ya Kati. Elizabeth James na Mulamba Mpepo. 0754-487781.

Hatuwezi kusema zinaridhisha kwa vile hakuna mabadiliko ya maana yaliyofanyika kama vile kuweka reli na mataluma, injini na mabehewa mapya na pia kuboresha masilahi ya wafanyakazi . Hamis Mumba, Singida 0712-055531.

Huduma zitolewazo na mwekezaji mpya wa Shirika la Reli haziridhishi! Kitendo cha kupunguza awamu za usafiri kutoka awamu nne hadi mbili za sasa kwa wiki ni moja ya upungufu wa mwekezaji huyo. Wananchi walitegemea mfumo mzima uboreshwe. Chiza Gwide UDSM. 0786-615090.

Ukweli ni kwamba hakuna mwekezaji anayekuja hapa nchini au katika Afrika kwa ajili ya kuinua uchumi wa nchi husika na wananchi wake kwa ujumla isipokuwa kila mmoja anazingatia faida zaidi . Josephat Kashendwa. 0717-724150.

Bahati mbaya sana mimi ni mtaalamu wa shughuli za reli, hivyo kwangu mimi kubinafsishwa kwa Shirika la Reli naona ni kejeli tu. 0787- 000044

MJADALA MPYA

Kukwama kwa mahujaji Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwenda kuhiji Makka katika muda muafaka, nani anapaswa kulaumiwa?

Tutumie maoni yako kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu (SMS) kupitia simu; 0782-698386. Ujumbe utakaoandikwa vizuri kwa lugha fasaha ndio utakaopewa kipaumbele - Mhariri.


h.sep
juu sp.b
Habari Mpya  |  Kitaifa  |  Dar  |  Mikoani  |  Tahariri  |  Makala  |  Michezo  |  Matangazo  |  Webmaster
Copyright 2007 © FreeMedia Ltd.
Free media limited
mtaa wa Mkwepu na Makunganya, jengo la Bilicanas, gorofa ya kwanza, SLP 15261, Dar es salaam, Tanzania
simu +255-22-2126233  •  faksi +255-22-2126234  •  Selula  0713 296570