MWANADAMU ni kiumbe pekee kati ya viumbe wengi duniani aliyekirimiwa karama na vipawa mbalimbali maishani mwake.
Kipawa kinachoonyesha tofauti ya binadamu na viumbe wengine ni utashi au hali ya kuweza kuchagua hili au lile baada ya kutafakari.
Hata hivyo kila kiumbe kina namna yake ya kujishughulisha na kujipatia mahitaji yake, na kina jinsi yake ya kujikinga na maadui.
Kila kiumbe hai kina namna yake ya kuhisi na kupata mahitaji yake. Chukua mfano wa mimea, kuna baadhi ya miti ikiguswa majani yake husinyaa kwa hujikunja na inapoachwa kuguswa hukunjuka.
Kwa wanyama pia, ndege na wadudu, hawa wana akili na katika maisha yao wana mipango yao. Wana viongozi wao, tujifunzeni hili kutoka kwa nyuki au mnyama kama simba, hawa wana viongozi wao wanaowaongoza katika maisha yao ya kila siku.
Ingawa binadamu ni kiumbe aliyestaarabika zaidi lakini kuna viumbe wengine wenye mstaarabu unaoweza kuwa zaidi ya ule wa binadamu.
Kwa mfano, wapo wanyama ambao wana heshimu sana kitendo cha kijamiiana, dume anapohitaji humnusa kwanza mwanamke na akigundua kuwa ule si wakati muafaka basi huendelea na safari yake bila kuleta taabu.
Hali hii ni tofauti kidogo kwa binadamu ambaye hana upeo wa kunusa na kutambua wakati unaofaa kwa tendo hilo.
Lakini pamoja na kushindwa kunusa bado mwanadamu katika utashi alionao ana bahati ya kufikiri na kupanga lipi la kufanya na kwa nini alifanye!
Hata hivyo, inashangaza kuona binadamu akifanya mambo mengine yasiyo na maana kwake na hata kwa jamii anayoishi.
Hili linaweza kuthibitishwa na mfano wa baadhi ya watu katika jamii yetu ambao wamekuwa na tabia ya kuiga tabia na desturi za wenzetu hukuwa wakijua kuwa wanachoiga ni kitu hatari.
Mifano katika hili ipo mingi kama kuiga namna ya uvaaji unaopendelewa zaidi na jamii za watu wa mataifa ya Magharibi, ulaji wao, namna ya kuzungumza na hata jinsi ya kufanya mapenzi.
Mengi ya haya tuyaigayo yana athari kubwa kwa maadili asilia ya kitanzania. Athari hizi sasa zimeanza kuonekana wazi katika jamii yetu kwa wazazi kuoga kukaa wakiwa watupu pamoja na watoto wao.
Tabii hii ni athari za kuiga staili ya maisha ya jamii ya watu wa Magharibi wanaopenda kwenda kwenye fukwe za bahari kuogolea pamoja na watoto wao, hivi sasa wapo baadhi yetu wanaoogolea katika fukwe na watoto wao wakiwa na mavazi ya ndani tu.
Yapo baadhi ya mambo yaliyoigwa kutoka jamii za Kimagharibi na jamii ikayakemea yakaachwa lakini yanafanywa na watanzania wakiwa nje ya mipaka ya nchi yetu.
Baadhi ya mambo hayo ni utaratibu unaotumika kumtafuta msichana mlimbwende wa dunia. Mabinti zetu hujianika na vichupi majukwaani, jambo lisilokubalika katika maadili ya Kitanzania.
Tupende tusipende, haya ni mambo tunayopaswa kuyapiga vita yasizidi kuenea katika jamii yetu.
Katika kupambana na tamaduni za kigeni zinazopingana na tamaduni zetu, tunapaswa kukemea zaidi kufanya mapenzi kwa staili ya Magharibi ambayo sasa inaonekana kupendwa zaidi ya vijana wetu.
Jamii za wenzetu wapenda zaidi kunyonyana ulimi, jambo hatari kwa afya binadamu. Mnaweza kuambukizana maradhi kama kifua kikuu.
Pengine nikumbushe kuwa kinywa ni shimo lililo chanzo cha bomba au mrija mrefu wa kupitisha aina mbalimbali za vyakula.
Vyakula hivi vikurundika pamoja kwa muda mrefu vinaoza na kutoa harufu isiyopendeza, na vyakula vya kujenga mwili (protein) kama maharage, nyama, na mayai ndivyo vinaongoza kwa kuharibika na kutoa harufu mbaya.
Vyakula hivi huichafua njia yote vinapopa, yaani kuanzia kinywani hadi mwisho tumboni. Kwa hali hiyo hata kama zoezi la kuoza kwa vyakula hivi linafanyika tumbo, kwa kuwa bomba linalopitisha chakula hicho liko wazi muda mrefu huweza kupandisha harufu kutoka tumboni hadi kinywani.
Hatari zaidi ipo mabinti zetu wanaofanyishwa biashara ya mapenzi kwa sababu wanalazimika kuyafanywa haya ili waweze kujikimu kimaisha. Kwa sababu hiyo, jamii yetu inapaswa kuwa makini kwa kuyoiga kila tamadamu za kigeni.
Kwa pamoja tunapaswa sasa kuanzisha vita kabambe ya kuzikataa tamaduni za kigeni zinazohatarisha afya zetu na kujenga misingi imara ya kuzikumbatia tamaduni zetu.