logo spc.r_ad0
sp.b_ad0
blu.strip
spc.bt_blu.strip
HABARI MPYA KITAIFA DAR MIKOANI TAHARIRI MAKALA MICHEZO
sp.b_menu
ban
sp.b_ban
jumapili, 16 Desemba 2007
Pekua Tovuti
sp.t_sech.box sp.tafuta_w_tuma sp.t_tuma sp.r_tuma
sp.b_box sp.b_tuma
sp.b_F1
h.sep1
sp.r_men
sp.t
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari
sp.b_tuma
sp.l_men
h.sep1
sp.l sp.t sp.r
LOGIN
sp.men.l sp.men.t sp.men.r
Username
sp.b_user
sp.t-word
Password
sp.b_word
sp.t_btn
sp.b_btn
sp.b
h.sep1


Rais Kikwete; sitaki kuamini
Mwandishi Wetu


NINAANDIKA kwa masikitiko, ninawasikitikia mahujaji, na hasa wazee, wanawake na watoto waliokuwa wakilala chini kwa takriban siku kumi wakisubiri safari yao ya kwenda kuhiji huko Makka.

Katika historia ya Tanzania, tukio la kukwamishwa kwa mahujaji kama lilivyotokea mwaka huu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa J. K. Nyerere, Dar es Salaam ni la kwanza na la aina yake.

Mahujaji waliokumbwa na mkasa huo ni zaidi ya 1,300 kutoka taasisi mbambali za dini ya Kiislamu zinazohusika na uratibu wa safari hizo kila mwaka. Miongoni mwa taasisi husika ni Tanzania Muslim Hajj Trust, Twayyibah, Al birri, BAKWATA, Istiqamaah n.k

Kabla ya ATCL kutaka kurejesha tena huduma zake, taasisi hizo zilikuwa zikiendelea tena kwa ufanisi mkubwa kupata huduma hiyo kupitia mashirika mengine ya ndege.

Katika hali ya kutaka kuimarisha uzalendo, mapema mwaka huu, taasisi hizo ziliitikia mwito wa ATCL baada ya kuziomba kutumia shirika hilo kwa lengo la kukuza soko lake nchini.

Kwa upande wao, taasisi za Kiislamu waliwezesha kutekeleza masharti yote kwa mahujaji na kwa ATCL kwa muda muafaka kiasi cha kuwafanya mahujaji na Waislamu wengi nchini kutaraji kuona safari ya hijja ya mwaka huu kuwa nzuri zaidi kuliko miaka ya nyuma.

Hali haikuwa hivyo kwa upande wa ATCL, mpaka siku ya mwisho ambayo mahujaji walitakiwa kuanza kuondoka bado walikuwa hawana maandalizi yoyote ya kuwasafirisha.

Jumatatu Desemba 12, ATCL ilitoa taarifa kuwa ndege iliyopangwa kuwasafirisha mahujaji ni mbovu, hivyo walitakiwa kusubiri hadi siku inayofuata, Desemba 4, lakini pia safari haikuwepo na hali iliendelea hivyo mpaka Desemba 13 walipoanza kuondoka.

Ni jambo la kusikitisha kwa sababu katika hali ya shaka na hofu, mahujaji wakiwa hawana hatia yoyote, walijikuta wakiadhibiwa kwa kuteseka uwanja wa ndege kwa siku kumi mfululizo huku wakibadilishiwa kila aina ya uongo juu ya kuwepo kwa safari yao.

Lakini jambo la kusikitisha katika sakata hili zima, ni usanii waliofanyiwa mahujaji wakati Rais Jakaya Kikwete alipowasili uwanjani hapo Desemba 11, tayari kupanda ndege kwenda zake Marekani.

Rais Kikwete akiwa pale uwanjani, kundi la mahujaji walichukuliwa na kupakizwa kwenye ndege wakielezwa kuwa safari yao ilikuwa imeiva. Rais alipewa fursa maalumu ya kuwaaga, akawaaga. Na waliobaki uwanjani walibaki na matumaini kuwa wakati wowote wangeondoka kwa sababu kundi la kwanza tayari lilikuwa safarini. Rais Kikwete naye akapanda zake ndege kuelekea Marekani.

Baada ya Kikwete kuondoka, mahujaji hao walishushwa kwenye ndege kwa maelezo kuwa ndege husika haina kibali cha kutua Jedda, nchini Saudi Arabia.

Wakati mahujaji wakipandishwa ndege ili waondoke, viongozi kadhaa waandamizi wa serikali walikuwepo na walishiriki kuwaaga huku wakiwatakia safari njema ya kwenda kutekeleza moja ya nguzo muhimu za dini ya Kiislamu.

Swali gumu na lenye kutatiza katika utata huu ni hili, hivi ni kweli ndege waliyopandishwa mahujaji haikuwa na kibali cha kutua Saudi Arabia? Na kama haikuwa nacho, maofisa husika wa uwanja wa ndege hawakulijua hili? Sitaki kuamini kama hawakuwa na taarifa sahihi kuhusu vibali vya ndege hiyo. Hakika sitaki kuamini!

Na kama hivyo ndivyo, inawezekana maofisa wa uwanja wa ndege walimdanganya Rais Kikwete kuhusu ndege hiyo kutokuwa na kibali cha kutua Saudi Arabia? Inawezekana kweli? Siamini.

Siamini kwa sababu ninajua hawawezi kumdanganya mkuu wa nchi katika jambo nyeti kama hilo. Hili nalo sitaki kuliamini kabisa!

Na zaidi hapa ni kwamba, sitaki kuamini kama shirika letu la ndege limefikia hatua ya kuingia kwenye mchezo mchafu wa kuigiza, kuigiza katika tukio kubwa la ibada kama hijja, tukio linalogusa imani za wananchi walio wengi. Ni tukio la aibu kwa serikali ambalo ni vigumu kuamini kama limetokea, ingawa ukweli unabaki pale pale kwamba limetokea!

Ngoja kidogo, nirejee baadhi ya mambo yalivyokuwa baada ya kuonekana kuwepo hali ya usanii katika safari hiyo. Baadhi ya mahujaji walionekana kuwa na furaha walipowaona viongozi wakuu wa nchi uwanjani pale – Rais Kikwete na Waziri Mkuu Edward Lowassa - wakiwahakikishia kuwepo kwa safari yao, japo si katika muda muafaka, lakini si kuendelea kusota pale.

Wapo pia walioamua kuondoka kwa kutumia ndege nyingine kwa gharama zingine kinyume na bajeti zao, baada ya kuona ubabaishaji uliokuwa ukifanyika uwanjani pale, tena mbele ya viongozi wa serikali, hii nayo ni aibu, ni ngumu kuamini, lakini ndio ukweli kama nilivyoeleza hapo juu.

Lakini cha kusikitisha na ambacho sitaki aslani kukiamini ni kama kweli Rais Kikwete mwenyewe au wasaidizi wake waliamua kuwahadaa mahujaji.

Hivi ni nani aliyempa Rais Kikwete taarifa kuwa ndege ile ina kibali cha kutua Saudi Arabia wakati kibali hicho hakikuwepo? Maswali ambayo majibu yake ni vigumu kuyaamini ni mengi.

Mimi siamini, kama Rais Kikwete binafsi alijua ukweli kuwa ndege ilikuwa haina kibali cha kutua Saudia, lakini kwa sababu zilizo nje ya uwezo wake akaamua kuwahadaa wananchi wake. Hili sitaki kuamini.

Rekodi ya Rais Kikwete haionyeshi kama amewahi kushiriki kutenda vitendo vya aina hii, ndiyo sababu sitaki kuamini. Lakini pamoja na kutoamini, ukweli ni kwamba Rais Kikwete ameaibika mbele ya macho ya mahujaji, na anapaswa kujisafisha.

Na dawa ya kujisafisha ni moja tu, ni kuwawajibisha wale wote waliompa taarifa zisizo sahihi kuhusu ndege hiyo hadi akadiriki kusimama mbele ya mahujaji na kuwaaga akiwatakia safari njema na wao wakimtakia safari njema ya Marekani.


h.sep
juu sp.b
Habari Mpya  |  Kitaifa  |  Dar  |  Mikoani  |  Tahariri  |  Makala  |  Michezo  |  Matangazo  |  Webmaster
Copyright 2007 © FreeMedia Ltd.
Free media limited
mtaa wa Mkwepu na Makunganya, jengo la Bilicanas, gorofa ya kwanza, SLP 15261, Dar es salaam, Tanzania
simu +255-22-2126233  •  faksi +255-22-2126234  •  Selula  0713 296570