logo spc.r_ad0
sp.b_ad0
blu.strip
spc.bt_blu.strip
HABARI MPYA KITAIFA DAR MIKOANI TAHARIRI MAKALA MICHEZO
sp.b_menu
ban
sp.b_ban
jumatatu, 18 Juni 2007
Pekua Tovuti
sp.t_sech.box sp.tafuta_w_tuma sp.t_tuma sp.r_tuma
sp.b_box sp.b_tuma
sp.b_F1
h.sep1
sp.r_men
sp.t
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari
sp.b_tuma
sp.l_men
h.sep1
sp.l sp.t sp.r
LOGIN
sp.men.l sp.men.t sp.men.r
Username
sp.b_user
sp.t-word
Password
sp.b_word
sp.t_btn
sp.b_btn
sp.b
h.sep1
tp.spc


VETA kuzalisha ajira zenye ushindani


na Joseph Malembeka, Kilosa


CHUO cha VETA Mikumi, kimeahidi kuzalisha ajira zenye ushindani katika soko la ajira Afrika Mashariki na Kati zaidi ya robo ya ajira 1,000,000 zinazokusudiwa kutolewa na serikali ya awamu ya nne ifikapo mwaka 2010.

Sambamba na ahadi hiyo, chuo hicho kimeihakikishia serikali kuwa, katika mfumo mahiri wa ufundishaji (CBET), kitazalisha wahitimu watakaoshinda soko huria la ajira Afrika Mashariki na Kati, huku wengine wakijiajiri bila kutatizwa na kukua kwa teknolojia na utandawazi.

Kaimu Mkurugenzi wa VETA Makao Makuu, Alois Shayo, alimweleza hayo Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Ludovick Mwananzila, aliyekwenda kutunuku vyeti kwa wahitimu 162 wa fani mbalimbali ikiwemo ya uongozaji watalii iliyoanza kutolewa hivi karibuni chuoni hapo.

“Mfumo wa CBET sambamba na utoaji vifaa vya kuanzia kazi kwa wahitimu unaotumiwa sasa na vyuo vya VETA nchini, unavifanya vyuo hivyo kuzalisha ajira badala ya wahitimu kama ilivyokuwa hapo awali,” alisema Shayo.

Awali, mkuu wa chuo hicho, Ramadhani Mataka, alimweleza Naibu Waziri huyo kuwa chuo hicho kinachoendesha mafunzo mbalimbali kwa muda mrefu na mfupi, tayari kimezalisha wahitimu zaidi ya 5,000 kati ya mwaka 2002 hadi 2007.

“Pia chuo kinafanya mazungumzo na vyuo vya juu hapa nchini, mfano Chuo cha Wanyama pori Mweka ili viwatambue na kuwaendeleza wahitimu wetu katika kiwango cha juu cha elimu kitakachowezesha kuwatoa wageni wanaokuja kutafuta ajira nchini mwetu,” alisema Mataka.

Alisema katika ajira hizo zinazotarajiwa kuzalishwa na chuo hicho kila mwaka, VETA Mikumi inakusudia kutoa wahitimu bora 1,700 wa fani ya uongozi wa watalii kwa mwaka ifikapo 2011.


h.sep

juu sp.b
Habari Mpya  |  Kitaifa  |  Dar  |  Mikoani  |  Tahariri  |  Makala  |  Michezo  |  Matangazo  |  Webmaster
Copyright 2007 © FreeMedia Ltd.
Free media limited
mtaa wa Mkwepu na Makunganya, jengo la Billicanas, gorofa ya kwanza, SLP 15261, Dar es salaam, Tanzania
simu +255-22-2126233  •  faksi +255-22-2126234  •  Selula  0713 296570