logo spc.r_ad0
sp.b_ad0
blu.strip
spc.bt_blu.strip
HABARI MPYA KITAIFA DAR MIKOANI TAHARIRI MAKALA MICHEZO
sp.b_menu
ban
sp.b_ban
jumanne, 19 Juni 2007
Pekua Tovuti
sp.t_sech.box sp.tafuta_w_tuma sp.t_tuma sp.r_tuma
sp.b_box sp.b_tuma
sp.b_F1
h.sep1
sp.r_men
sp.t
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari
sp.b_tuma
sp.l_men
h.sep1
sp.l sp.t sp.r
LOGIN
sp.men.l sp.men.t sp.men.r
Username
sp.b_user
sp.t-word
Password
sp.b_word
sp.t_btn
sp.b_btn
sp.b
h.sep1
tp.spc


Wabunge waibana serikali


na Kulwa Karedia, Dodoma


KAMA ilivyotarajiwa, wabunge wengi walioanza kuchangia bajeti ya 2007/08 jana jioni, wameonyesha kutoridhishwa kwao na ongezeko la ushuru katika bidhaa za mafuta ya aina zote.

Wakichangia mjadala wa bajeti iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha Zakia Meghji, Alhamisi iliyopita, wabunge hao, wakiwamo wa upinzani na wale wa chama tawala, walisema kuwa bajeti hiyo imezidi kuwakandamiza wananchi na kwamba hatua za makusudi zinapaswa kuchukuliwa ili kunusuri hali hiyo.

Mbunge wa Karatu, Willbroad Slaa (CHADEMA), alisema hakuna sababu ya wananchi kufunga mkanda kwa madai kuwa hali ya uchumi ni mbaya, kwani mipango mibovu iliyowekwa ndiyo imechangia hali hiyo.

Alisema kutokana na serikali kupandisha kodi ya mafuta, sasa kuna hatari ya wamiliki wa mabasi kupandisha nauli maradufu, wauzaji wa nguo nao kuongeza bei, vitendo ambavyo vitazidi kuwaumiza wananchi.

Alisema Bunge linao uwezo mkubwa wa kukubaliana ili kutengua uamuzi wa serikali kupandisha kodi kwenye mafuta.

Alisema serikali imeshindwa kuonyesha makucha yake katika kudhibiti matumizi ya fedha zake, hali ambayo imechangia matatizo makubwa.

Alisema serikali imeshindwa kutoa ufafanuzi wa Kampuni ya Meremeta ambayo ilianzishwa na hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, kwa lengo la kusaidia jeshi, lakini vivi sasa inatumika kuneemesha vigogo.

Huku akitoa vielelezo, Dk. Slaa alisema ujenzi wa majengo mapya ya Benki Kuu ya Tanzania, umehusishwa na vitendo vya rushwa na kwamba serikali inapaswa kutoa maelezo ya kina juu ya suala hilo.

“Nimepata ujumbe wangu kwenye E-mail kupitia mtandao wa Peter Junior 1980@yahoo.com, ukimhusisha Gavana wa Benki Kuu, Daud Balali na kashfa ya ujenzi wa majengo mapya ya benki hiyo,” alisema.

Mbali na hali hiyo, Slaa alisema kuwa yuko tayari kukatwa posho yake ya kila siku ili kuchangia kodi ya mafuta kwa lengo la kuwapunguzia wananchi mzigo.

Mbunge wa Ukerewe, Getrude Mongella (CCM), naye alionyesha kutoridhishwa na na kusema wazi kuwa bajeti hiyo ni ngumu na wala si nyepesi kama ilivyokuwa mwaka jana.

“Watu wanalalamika sana juu ya bajeti hii kwani kawaida kunapokuwepo na bajeti na kibaya zaidi ikiwa imewabana sana, lazima watoe kilio chao,” alisema Mongella.

Alisema bajeti hiyo imeonyesha wazi kuwa serikali iko katika hali ngumu ya kifedha kitendo ambacho sasa viongozi wa serikali wanapaswa kwenda kuwaeleza ukweli wananchi.

Aliionya serikali kujenga utamaduni wa kuweka nidhamu ya matumizi ya fedha za walipa kodi na kutoa ukweli wa hali ya matumizi ya fedha hizo katika miradi inayokusudiwa.

“Wakati wa vita ya uvamizi wa nduli Idd Amin mwaka 1978 tuliambiwa tufunge mikanda na tukafanya hivyo kwa uvumilivu lakini kwa sasa suala hili wananchi watataka kupewa maelezo ya kina,” alisema Mongella.

Aliwataka wabunge wasikubali kufunga mikanda bila kuhoji fedha zilizotumwa na serikali zimefanya nini.

Alionyesha kusikitishwa kwake na serikali kushindwa hata kununua gari la zimamoto katika Mkoa wa Singida, ambako juzi kulitokea ajali ya basi la Mohamed Trans na kuua watu wanaokadiriwa kufikia 25.

Naye Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo (UDP), alisema alitegemea bajeti hiyo ingekuwa mkombozi wa wananchi lakini imeshindwa kuonyesha matumaini.

“Jimboni kwangu tulijenga shule 28 za sekondari baada ya agizo la serikali, ujenzi huu ulihusisha wananchi kutoa michango, kuchapwa viboko ili azima ya serikali itimie, sasa hakuna sehemu inayoonyesha kuwa itaisaidia kujenga vyumba vya madarasa,” alisema Cheyo.


h.sep

juu sp.b
Habari Mpya  |  Kitaifa  |  Dar  |  Mikoani  |  Tahariri  |  Makala  |  Michezo  |  Matangazo  |  Webmaster
Copyright 2007 © FreeMedia Ltd.
Free media limited
mtaa wa Mkwepu na Makunganya, jengo la Billicanas, gorofa ya kwanza, SLP 15261, Dar es salaam, Tanzania
simu +255-22-2126233  •  faksi +255-22-2126234  •  Selula  0713 296570