logo spc.r_ad0
sp.b_ad0
blu.strip
spc.bt_blu.strip
HABARI MPYA KITAIFA DAR MIKOANI TAHARIRI MAKALA MICHEZO
sp.b_menu
ban
sp.b_ban
jumanne, 19 Juni 2007
Pekua Tovuti
sp.t_sech.box sp.tafuta_w_tuma sp.t_tuma sp.r_tuma
sp.b_box sp.b_tuma
sp.b_F1
h.sep1
sp.r_men
sp.t
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari
sp.b_tuma
sp.l_men
h.sep1
sp.l sp.t sp.r
LOGIN
sp.men.l sp.men.t sp.men.r
Username
sp.b_user
sp.t-word
Password
sp.b_word
sp.t_btn
sp.b_btn
sp.b
h.sep1
tp.spc


Sitta awaonya wabunge


na Kulwa Karedia, Dodoma


SPIKA wa Bunge, Samuel Sitta, amewaonya wabunge kuacha kutumia lugha isiyoeleweka wakati wa vikao vya Bunge.

Spika Sitta alifikia hatua hiyo ya kuwaonya wabunge jana baada ya Mbunge wa Mji Mkongwe Ibrahim Sanya (CUF), kutumia maneo ya lugha ya Kiswahili yasiyokuwa rasmi.

Sanya alitumia maneno hayo wakati akiuliza swali la nyongeza kufuatia swali lake la msingi alipotaka kujua ni wakati gani muafaka wa kuandaa utaratibu mzuri wa kutoa vibali maalumu kwa vijana.

Kutokana na lugha hiyo, Spika Sitta alimkatisha mbunge huyo na kusema kuwa sasa kumeibuka mambo mengi ndani ya Bunge.

Sanya alitumia neno mwiba wa mchongoma, akinaamisha kwamba vijana wengi wanaofanya biashara zao huko Zanzibar wamekuwa wakibanwa zaidi.

“Kumekuwa na maneno yanayotumika hivi sasa, Mheshimiwa Sanya naona hili si swali, na neno mwiba wa mchongoma si neno zuri la kutumia,” alisema Sitta na kumkatisha kuendelea na swali lake.

Alisema bungeni ni sehemu muhimu ambako hujadiliwa mambo mazito kwa ajili ya manufaa ya wananchi na kwamba kama kuna jambo lazima litolewe kwa hoja.

“Napenda kutoa tahadhari ya awali kwa wabunge wote juu ya lugha inayotumika, sasa hivi kumekuwa na mambo mengi kuhusu bajeti hii, utasikia bei zimepanda, bajeti maumivu tupu,” alisema Sitta.

Kutokana na hali hiyo, Sitta alifuta swali hilo na kuendelea na utaratibu mwingine.


h.sep

juu sp.b
Habari Mpya  |  Kitaifa  |  Dar  |  Mikoani  |  Tahariri  |  Makala  |  Michezo  |  Matangazo  |  Webmaster
Copyright 2007 © FreeMedia Ltd.
Free media limited
mtaa wa Mkwepu na Makunganya, jengo la Billicanas, gorofa ya kwanza, SLP 15261, Dar es salaam, Tanzania
simu +255-22-2126233  •  faksi +255-22-2126234  •  Selula  0713 296570