logo spc.r_ad0
sp.b_ad0
blu.strip
spc.bt_blu.strip
HABARI MPYA KITAIFA DAR MIKOANI TAHARIRI MAKALA MICHEZO
sp.b_menu
ban
sp.b_ban
jumanne, 19 Juni 2007
Pekua Tovuti
sp.t_sech.box sp.tafuta_w_tuma sp.t_tuma sp.r_tuma
sp.b_box sp.b_tuma
sp.b_F1
h.sep1
sp.r_men
sp.t
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari
sp.b_tuma
sp.l_men
h.sep1
sp.l sp.t sp.r
LOGIN
sp.men.l sp.men.t sp.men.r
Username
sp.b_user
sp.t-word
Password
sp.b_word
sp.t_btn
sp.b_btn
sp.b
h.sep1
tp.spc


Stars haijapata kutokea


na Mwandishi Wetu


HAKIKA, haijapata kutokea, wachezaji wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, jana walichangiwa jumla ya sh mil. 322.5 katika harambee iliyosimamiwa na Waziri Mkuu, Edward Lowassa, mjini Dodoma.

Akitangaza mara baada ya harambee hiyo iliyofanyika wakati wa chakula cha mchana kilichoandaliwa kwa ajili ya timu hiyo katika Hoteli ya Dodoma, mjini hapa, Waziri Mkuu alisema, fedha hizo zinaweza kuwa msaada mkubwa kwa wachezaji hao badala ya kuzitafuna kwa starehe.

Mara baada ya kupewa changamoto hiyo, aliinuka Naibu wa Waziri wa Michezo na Utamaduni wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mahmoud Thabit Kombo, aliyekuwa mkuu wa msafara kwa upande wa serikali na kusema, azima ya wachezaji ni fedha hizo kujengewa nyumba kupitia mifuko ya kijamii kama vile NSSF.

“Mhe. Waziri Mkuu tukiwa njiani kutoka bungeni, vijana wamejadili suala hilo na kuamua kuwa wakipata kama sh mil. 200 watawekeza ili zitafutwe njia mahususi za kuwasaidia wajenge nyumba… au hata kununua magari.”

Waziri Mkuu, aliwashauri wawasiliane na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau, ambaye alikuwapo katika hafla hiyo ili waangalie ni namna gani fedha zao zinaweza kutumika kwa manufaa zaidi.

Alisema, bungeni wamepata sh milioni 33 kutoka kwa wabunge wote, yeye Lowassa amepata sh mil. 47 kutoka kwa watu wanne tofauti na wizara, huku Wizara ya Miundombinu imeahidi kutoa sh mil. 70, hivyo jumla ni sh mil. 150.

Hivyo, aliwataka mawaziri waliokuwapo katika hafla hiyo fupi, nao wachangie ili kuwasaidia vijana hao watimize azima yao.

Wa kwanza kuchangia alikuwa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge ambaye alisema wizara yake na taasisi zilizo chini yake, wanaongeza sh mil. 30.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe, alisema wizara yake na makampuni yaliyo chini yake, watatoa sh mil. 30.

Ahadi nyingine zilitolewa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Basil Mramba (sh mil 30); Waziri wa Kazi Ajira na Vijana, John Chiligati, (sh mil. 10) na Waziri wa Nishati na Madini, Naziri Karamagi (sh mil 15).

Mbali ya kiasi hicho, Karamagi aliahidi kutoa sh mil. 15 kutoka kwenye makampuni yake binafsi.

Michango mingine ilitolewa na Mbunge wa Singida Mjini, Mohammed Dewji (sh mil. 30); mmiliki wa Kampuni ya TIOT ambaye ametoa pesa taslimu sh mil. 10 ambazo waliahidiiwa kukabidhiwa mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam huku wakazi wa Dodoma wakichanga kiasi cha sh mil 2.5 ambazo kapteni wa timu hiyo, Shadrack Nsajigwa, alizipokea kwa niaba ya wenzake kutoka kwa waziri mkuu.

Akizungumza mara baada ya harambee hiyo, Kocha wa timu hiyo, Marcio Maximo, alimweleza waziri mkuu kwamba wachezaji wa Tanzania wanapokuwa uwanjani wanacheza na watu 22 badala ya watu 11.

“Kwa wenzetu kutoka nchi zilizoendelea, hawana wasiwasi wanapokuwa uwanjani kwa sababu wana uhakika na maisha yao, na hivyo anapokuwa uwanjani akili inakuwa imetulia.

“Lakini hawa vijana ambao leo hii tunawaita mashujaa, wanacheza na watu 11, huku wakiwa na watu baki, ambayo ni mawazo na matatizo kuhusu familia zao.”

“Waulize hawa hapa …wanapanda daladala kuja mazoezini, hawana hata magari, wengine hata vyumba vya kulala wanachangia na wenzao kwa sababu hawawezi kumudu kodi…,” alisema huku akishangiliwa na wachezaji hao.

Alisema, anawashukuru sana Watanzania wote kwa kuwatia moyo wachezaji wake na kwa mapokezi waliyoyapata tangu warejee nchini jana, na kuongeza kuwa ana imani kubwa na vijana wake.

Hii yote ni baada ya timu hiyo kuwapa raha Watanzania baada ya kushinda bao 1-0 dhidi ya Burkina Faso juzi.

Mechi hiyo, ni katika harakati za kusaka tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mapema mwakani nchini Ghana.

Kwa ushindi wa juzi, Stars inakamata nafasi ya pili katika kundi la saba kwa kuwa na pointi nane kama kinara Senegal, lakini ikiwa na wastani mzuri wa mabao.

Katika mechi ya mwisho ya Septemba 8, itakayopigwa nchini dhidi ya Msumbiji, ndiyo itaamua hatima ya Stars kwenda Ghana au la.


h.sep

juu sp.b
Habari Mpya  |  Kitaifa  |  Dar  |  Mikoani  |  Tahariri  |  Makala  |  Michezo  |  Matangazo  |  Webmaster
Copyright 2007 © FreeMedia Ltd.
Free media limited
mtaa wa Mkwepu na Makunganya, jengo la Billicanas, gorofa ya kwanza, SLP 15261, Dar es salaam, Tanzania
simu +255-22-2126233  •  faksi +255-22-2126234  •  Selula  0713 296570