logo spc.r_ad0
sp.b_ad0
blu.strip
spc.bt_blu.strip
HABARI MPYA KITAIFA DAR MIKOANI TAHARIRI MAKALA MICHEZO
sp.b_menu
ban
sp.b_ban
jumanne, 19 Juni 2007
Pekua Tovuti
sp.t_sech.box sp.tafuta_w_tuma sp.t_tuma sp.r_tuma
sp.b_box sp.b_tuma
sp.b_F1
h.sep1
sp.r_men
sp.t
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari
sp.b_tuma
sp.l_men
h.sep1
sp.l sp.t sp.r
LOGIN
sp.men.l sp.men.t sp.men.r
Username
sp.b_user
sp.t-word
Password
sp.b_word
sp.t_btn
sp.b_btn
sp.b
h.sep1
tp.spc


Wanahabari wang’ara Miss Ukonga 2007


na Schola Athanas na Shabani Mpalule


WAANDISHI wa habari, Mariam Nkya, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo cha Uandishi wa Habari, Dar es Salaam School of Journalism (DSJ), na Safina Kassanga wa Kampuni ya Mwananchi Communications, juzi usiku waling’ara katika kinyang’anyiro cha Miss Ukonga 2007.

Wanahabari hao waliwapeleka puta washiriki wengine, na Nkya kutawazwa kuwa malkia mpya wa kitongoji hicho, huku Kassanga akitwaa nafasi ya tatu, katika shindano lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa Free Time Resort, uliopo Ukonga jijini Dar es Salaam.

Katika mtanange huo, nafasi ya pili ilikwenda kwa Emmy Mtangi, wakati nafasi ya nne ilichukuliwa na mrembo Winfrida Joseph, nafasi ya tano ilishikwa na Hellen Lyimo.

Zawadi zilizotolewa katika shindano hilo ni pamoja na sh 200,000, kompyuta, nafasi ya kusoma kozi ya kompyuta pamoja na kufanya kazi katika idara ya matangazo na biashara katika Kampuni ya Uhuru Publications kwa mshindi wa kwanza.

Mshindi wa pili alipata sh 150,000, pamoja na seti moja ya luninga, huku mshindi wa tatu hadi wa tano walipewa kiasi cha sh 100,000 kila mmoja, wakati washiriki waliobaki walipewa kifuta jasho cha sh 40,000 kila mmoja.

Asia Idarous, ambaye ni mbunifu wa mitindo na mavazi, na mmiliki wa Kampuni ya Febark Fashion, ametoa zawadi ya kuwashonea mavazi watakayotumia warembo hao, katika kinyang'anyiro cha Miss Ilala, baadaye mwaka huu.


h.sep

juu sp.b
Habari Mpya  |  Kitaifa  |  Dar  |  Mikoani  |  Tahariri  |  Makala  |  Michezo  |  Matangazo  |  Webmaster
Copyright 2007 © FreeMedia Ltd.
Free media limited
mtaa wa Mkwepu na Makunganya, jengo la Billicanas, gorofa ya kwanza, SLP 15261, Dar es salaam, Tanzania
simu +255-22-2126233  •  faksi +255-22-2126234  •  Selula  0713 296570