logo spc.r_ad0
sp.b_ad0
blu.strip
spc.bt_blu.strip
HABARI MPYA KITAIFA DAR MIKOANI TAHARIRI MAKALA MICHEZO
sp.b_menu
ban
sp.b_ban
jumatatu, 13 Agosti 2007
Pekua Tovuti
sp.t_sech.box sp.tafuta_w_tuma sp.t_tuma sp.r_tuma
sp.b_box sp.b_tuma
sp.b_F1
h.sep1
sp.r_men
sp.t
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari
sp.b_tuma
sp.l_men
h.sep1
sp.l sp.t sp.r
LOGIN
sp.men.l sp.men.t sp.men.r
Username
sp.b_user
sp.t-word
Password
sp.b_word
sp.t_btn
sp.b_btn
sp.b
h.sep1
tp.spc


Polisi wawili mbaroni uporaji NMB Mwanga


na Charles Ndagulla, Moshi


ASKARI wawili wa kike (WP) wa Jeshi la Polisi nchini, wanashikiliwa kwenye vituo tofauti vya polisi mkoani Kilimanjaro wakihusishwa kupanga njama zilizofanikisha uporaji wa sh 239,260,000 kwenye Benki ya NMB tawi la Mwanga, mapema mwezi uliopita.

Kukamatwa kwa askari hao, kunafanya idadi ya polisi wanaoshikiliwa kuhusu tukio hilo kufikia wanne, akiwamo askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Monduli, mkoani Arusha na mmoja wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Mwanga.

Habari za uhakika zilizopatikana mwishoni mwa wiki kutoka ndani ya Jeshi la Polisi, zimethibitisha kukamatwa kwa askari hao wa kike, ambao wapo rumande kwa muda wa zaidi ya wiki moja sasa.

Kukamatwa kwa askari hao kunatokana na wao (askari) kushindwa kuwa waaminifu katika fungu la sh milioni 10 waliloelekezwa na watuhumiwa kwenda kuchukua mahali ambako fedha hizo zilikuwa zimechimbiwa chini mkoani Arusha.

Inadaiwa mmoja wa askari hao alisafiri hadi zilikofichwa fedha hizo na kufanikiwa kuzichukua akiongozwa na ramani aliyokuwa amepewa na watuhumiwa.

Watoa habari wanadai kuwa, askari huyo akielewa kuwa yu peke yake katika dili hilo, ghafla mwenzake alihoji kama amefanikiwa kuchukua kiasi hicho cha fedha.

Inadaiwa kuwa askari hao walishikwa na mshawasha baada ya kuona kiasi hicho kikubwa cha fedha, hivyo kugawana bila kuwafikishia walengwa.

Baada ya wahutumiwa hao wa kike ambao ni Watanzania kuona fungu hilo haliwafikii, huku wakiendelea kusota mahabusu bila kuelewa hatma yao, ndipo waliamua kufa na askari hao kwa kutoboa siri iliyojificha.

Mmoja wa askari hao anadaiwa kukutwa amefungua akaunti mpya kwenye moja ya benki hapa mkoani Kilimanjaro (NBC) hali ambayo inazidi kuwapa wasiwasi polisi wenzake.

Mbali na hilo, askari hao wanadaiwa kukutwa na kiasi kikubwa cha fedha majumbani mwao hali ambayo inadaiwa si kawaida yao.

Pamoja na kushikiliwa kwa muda wa wiki moja kwa askari hao, Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro, limeendelea kuweka usiri mkubwa kwa kutotoa majina ya watuhumiwa wanaoshikiliwa kuhusiana na tukio hilo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Lucas Ng’hobko, ameweka wazi msimamo wake wa kutotaja majina ya watuhumiwa akidai kuwa kuwataja kunaweza kuharibu upelelezi.

Tangu tukio hilo la uporaji litokee, Julai 11, mwaka huu na kusababisha mauji ya Askari PC. Michael aliyepigwa risasi kichwani na majamabazi hao, watuhumiwa bado wanaendelea kushikiliwa bila kufikishwa mahakamani.

Polisi pia inawashikilia raia wawili kutoka nchi jirani ya Kenya; Samwel Gitau Saitoti (30) anayeishi eneo la Ngong jijini Nairobi na Michael Kimani au Joachim (30), mkazi wa Thika nchini humo.

Watuhumiwa hao ni wale waliopambana na polisi kwa zaidi ya saa tano eneo la Njiro Kontena mkoani Arusha wakiwa na silaha za kivita, yakiwamo mabomu.

Katika tukio hilo, polisi walifanikiwa kukamata silaha tisa zikiwamo bunduki mbili aina ya SMG, bastola saba na risasi 128 zinazodaiwa kutumiwa katika tukio hilo la Mwanga.

Jeshi la Polisi nchini tayari limetoa idadi ya watu 20 wanaoshikiliwa mkoani Kilimanjaro wakihusishwa na uporaji katika benki hiyo, wakiwamo wanawake watano, ambao wote ni Watanzania.

Mkoani Kilimanjaro, Jeshi la Polisi lilikamata bastola mbili na magazine mbili za bunduki aina ya SMG, zikiwa na risasi 30 pamoja na risasi 18 ambazo zilikutwa kwenye soksi za mmoja wa watuhumiwa aliyeuawa na polisi.

Katika tukio hilo, polisi nao walifanikiwa kumuua jambazi mmoja aliyekuwa ndani ya gari dogo lenye namba za usajili T 979 AMY Toyota Corolla 100 katika mapambano ya kurushiana risasi eneo la YMCA mjini hapa.

Wakati huohuo, imebainika kuwa, makoti maalumu yasiyopenya risasi yanayodaiwa kukamatwa kwa watuhumiwa hao mkoani Arusha, ni ya kivita na yamekuwa yakitumiwa na majeshi ya NATO.

Moja ya koti hilo linadaiwa kuwa na uzito wa kilo 15, jambo ambalo linaelezwa na wataalamu wa masuala ya silaha kuwa, ni vigumu risasi kupenya hata kama imerushwa kutoka umbali mfupi.


h.sep

juu sp.b
Habari Mpya  |  Kitaifa  |  Dar  |  Mikoani  |  Tahariri  |  Makala  |  Michezo  |  Matangazo  |  Webmaster
Copyright 2007 © FreeMedia Ltd.
Free media limited
mtaa wa Mkwepu na Makunganya, jengo la Bilicanas, gorofa ya kwanza, SLP 15261, Dar es salaam, Tanzania
simu +255-22-2126233  •  faksi +255-22-2126234  •  Selula  0713 296570