logo spc.r_ad0
sp.b_ad0
blu.strip
spc.bt_blu.strip
HABARI MPYA KITAIFA DAR MIKOANI TAHARIRI MAKALA MICHEZO
sp.b_menu
ban
sp.b_ban
jumatatu, 28 Januari 2008
Pekua Tovuti
sp.t_sech.box sp.tafuta_w_tuma sp.t_tuma sp.r_tuma
sp.b_box sp.b_tuma
sp.b_F1
h.sep1
sp.r_men
sp.t
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari
sp.b_tuma
sp.l_men
h.sep1
sp.l sp.t sp.r
LOGIN
sp.men.l sp.men.t sp.men.r
Username
sp.b_user
sp.t-word
Password
sp.b_word
sp.t_btn
sp.b_btn
sp.b
h.sep1
tp.spc


Vyuo vikuu vyatakiwa kuboresha mitaala


na Chalila Kibuda


VYUO vikuu nchini vimetakiwa koboresha mitaala ya elimu kwa wanafunzi wa elimu ya juu, ili kuwawezesha wanafunzi kuingia kwenye soko la ajira.

Hayo yalielezwa mwishoni mwa wiki na Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge), Dk. Batrida Burian, kwa niaba ya Waziri Mkuu, wakati wa mahafali ya kwanza ya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT).

Burian alisema nchi zilizoendelea zimewekeza kwenye elimu na kupata wasomi wengi na kufungua milango ya uchumi wa nchi.

“Ninaamini taaluma mliyoipata mtaitumia vizuri katika maendeleo yenu wenyewe na taifa kwa ujumla, kwa kuonyesha ubora wa taaluma ya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam,” alisema Waziri Burian.

Alisema Tanzania inatakiwa kuwekeza kwenye elimu zaidi kuweza kutambulika kwa kuwa na wataalamu wengi.

Aidha, aliwasihi wahitimu kutokuwa chanzo cha maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU).

Naye Waziri wa Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Peter Msolla, alisema kwa sasa Tanzania haina wataalamu wa madini, lakini jitihada zinaendelea kuazisha kitengo hicho, ili kuweza kuwapata wataalamu hapa hapa nchini.


h.sep

juu sp.b
Habari Mpya  |  Kitaifa  |  Dar  |  Mikoani  |  Tahariri  |  Makala  |  Michezo  |  Matangazo  |  Webmaster
Copyright 2008 © FreeMedia Ltd.
Free media limited
mtaa wa Mkwepu na Makunganya, jengo la Bilicanas, gorofa ya kwanza, SLP 15261, Dar es salaam, Tanzania
simu +255-22-2126233  •  faksi +255-22-2126234  •  Selula  0713 296570