TANZANIA imetoka kapa Algeria kwenye mashindano ya ndondi za ridhaa kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya Olimpiki inayofanyika Algiers, Algeria.
Bondia pekee aliyebeba matumaini ya Tanzania, Hashim Simon naye alipondwa na Ramadhani Elwa wa Misri kwa pointi 24-2, habari hizo ni kwa mujibu wa Rais wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania (BFT), Shabani Mintanga.
Bondia huyo aliyecheza ndondi hizo kwa uzani wa Light Welter, alitolewa katika hatua ya robo fainali katika mashindano hayo ambayo kwa wanamichezo wanaofanya vema watashiriki katika mshindano ya Olimpiki yatakayofanyika Agosti, mwaka huu.
Kuondolewa huko kwa Simon kunafanya aungane na Watanzania wenzake akiwamo nahodha, Emillian Patrick (Bantum) na Leonard Machichi (Middle) waliotolewa mapema wiki iliyopita.