logo spc.r_ad0
sp.b_ad0
blu.strip
spc.bt_blu.strip
HABARI MPYA KITAIFA DAR MIKOANI TAHARIRI MAKALA MICHEZO
sp.b_menu
ban
sp.b_ban
jumanne, 29 Januari 2008
Pekua Tovuti
sp.t_sech.box sp.tafuta_w_tuma sp.t_tuma sp.r_tuma
sp.b_box sp.b_tuma
sp.b_F1
h.sep1
sp.r_men
sp.t
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari
sp.b_tuma
sp.l_men
h.sep1
sp.l sp.t sp.r
LOGIN
sp.men.l sp.men.t sp.men.r
Username
sp.b_user
sp.t-word
Password
sp.b_word
sp.t_btn
sp.b_btn
sp.b
h.sep1
tp.spc


Kesi ya Balozi Mahalu yaanza kunguruma


na Nuru Yanga


KESI ya kuhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Costa Mahalu, imeanza kusikilizwa jana na imeelezwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden anatarajiwa kutoa ushahidi katika kesi hiyo.

Habariza uhakika zilizopatikana nje ya mahakama zimeeleza kuwa balozi huyo ni miongoni mwa mashahidi 11 wanaotarajiwa kutoa ushahidi wao kwa upande wa mashitaka katika kesi hiyo.

Katika kesi hiyo, Mahalu na mfanyakazi mwingine wa ubalozi huo, Grace Martin, wanakabiliwa na makosa matano ya kula njama, kutenda kosa, kutumia nyaraka, kuiba na kuisababishia Serikali ya Tanzania hasara ya euro 3,098,741.40.

Jumla ya vipengele 26 vilisomwa katika maelezo ya awali na Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Tabu Mzee, mbele ya Hakimu Mkuu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, Sivangilwa Mwangesi, wakati kesi hiyo ilipoanza kusikilizwa.

Baadhi ya vipengele alivyovikubali ni kwamba Mahalu alikuwa balozi anayeiwakilisha Serikali ya Tanzania na pia alikiri kuwa matumizi yote ya fedha yalikuwa chini yake.

Pia alikiri kuwa mkataba wa kununua jengo hilo umeshuhudiwa na kamishna wa kiapo kwa mujibu wa sheria za Italia.

Miongoni mwa vipengele alivyovikana ni pamoja na kuiwakilisha Tanzania katika masuala ya kimataifa katika nchi za Italia, Ugiriki, Uturuki, Albani Serbia, Montenegro, Bosnia, Herzegovina na Slovenia.

Pia amekana kuomba na kupokea euro 3,078,741.40 katika mwaka wa fedha 2001/2002 na 2002/2003. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 27, mwaka huu.


h.sep

juu sp.b
Habari Mpya  |  Kitaifa  |  Dar  |  Mikoani  |  Tahariri  |  Makala  |  Michezo  |  Matangazo  |  Webmaster
Copyright 2008 © FreeMedia Ltd.
Free media limited
mtaa wa Mkwepu na Makunganya, jengo la Bilicanas, gorofa ya kwanza, SLP 15261, Dar es salaam, Tanzania
simu +255-22-2126233  •  faksi +255-22-2126234  •  Selula  0713 296570