HABARI MPYA KITAIFA DAR MIKOANI TAHARIRI MAKALA MICHEZO
jumatatu, 3 novemba 2008
Pekua Tovuti
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari


Wastaafu EAC kumjadili Kikwete leo


na Deogratius Temba


WASTAAFU wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC), leo wanakusanyika kuitafakari hotuba ya Rais Jakaya Kikwete, waliyosema imeonyesha dharau kwao kwa madai kuwa haikutoa suluhisho la matatizo yao ya muda mrefu.

Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana, Mwenyekiti wa wazee hao, Nathaniel Mlaki, alisema wastaafu hao wanakutana katika viwanja vya Mnazi Mmoja leo kuanzia saa 3, kujadili hatima ya malipo yao.

“Tumeshituka sana, kuona rais hajaguswa matukio yote ya wazee hawa kulala Ikulu, kufunga barabara, kwa hiyo tumeona tukusanyike, tujadili na kutoa uamuzi,” alisema Mlaki.

Alisisitiza kuwa wazee hao wameshitushwa na kauli Rais Kikwete kwamba ameamua kuliacha suala hilo litolewe tamko na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustapha Mkulo, kwani waziri huyo hana jipya kwa sababu alishatoa msimamo wake kwamba wastaafu hao, hawastahili kulipwa.

“Waziri alishasema hatustahili kulipwa na tamko lake la Oktoba 27 tunalo, leo rais anamwambia atoe tamko gani tena?” Tutashangaa kusikia tamko jipya kutoka kwa Mkulo. Hapa rais naye ameamua kutulisha pipi, sasa tutakutana kuweka mikakati yetu,” alisema.

Wiki iliyopita wasfaafu hao walileta usumbufu mkubwa baada ya kuamua kulala barabarani, huku wengine wakitoa nguo, kwa madai ya kuishinikiza serikali iwalipe madai yao.

Kutokana na kosa hilo, viongozi wa wastaafu hao, walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kosa la kulala barabarani na kufanya mkusanyiko kinyume cha sheria.


juu

Warning: mysql_connect() [function.mysql-connect]: Can't connect to local MySQL server through socket '/var/run/mysqld/mysqld.sock' (2) in /hermes/bosweb/web098/b983/glo.freemanm2/include/comment.php on line 9
I cannot connect to the database because: Can't connect to local MySQL server through socket '/var/run/mysqld/mysqld.sock' (2)