logo spc.r_ad0
sp.b_ad0
blu.strip
spc.bt_blu.strip
HABARI MPYA KITAIFA DAR MIKOANI TAHARIRI MAKALA MICHEZO
sp.b_menu
ban
sp.b_ban
ijumaa, 15 Februari 2008
Pekua Tovuti
sp.t_sech.box sp.tafuta_w_tuma sp.t_tuma sp.r_tuma
sp.b_box sp.b_tuma
sp.b_F1
h.sep1
sp.r_men
sp.t
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari
sp.b_tuma
sp.l_men
h.sep1
tp.spc


Wadau waombwa kuchangia taasisi ya Amina Chifupa


na Bethsheba Godson na Daniel Misheto


KAIMU Katibu wa Taasisi ya Amina Chifupa, Hassan Chifupa, amewaomba wale wote wenye mapenzi mema na marehemu Amina wasaidie kuchangia mfuko huo ili ukamilishe majukumu yake.

Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dar es Salaam, Chifupa alisema lengo la taasisi hiyo ni kuenzi yale yote marehemu Amina aliyokuwa akiyafanya kwa masilahi ya taifa.

Akifafanua, alisema baadhi ya mambo aliyokuwa akiyafanya ni kupiga vita mihadarati, kuendeleza michezo, kutoa misaada kwa watoto wanaoishi katika maisha magumu na mengineyo mengi.

Mzee Hamisi Chifupa, baba mzaza wa marehemu Amina Chifupa, aliyekuwa mbunge wa Viti Maalum (CCM), aliwasihi wabunge na madiwani waliofanya kazi na marehemu, nao kuchangia taasisi hiyo kama ishara ya kumuenzi marehemu.

Alisema michango hiyo itapokelewa kutumia akaunti ya taasisi hiyo Na. 01J1014153400 iliyopo Benki ya CRDB au fedha taslimu italipiwa katika ofisi yake iliyopo jengo la Uchumi Project, Barabara ya Shekilango karibu na Chuo cha Ustawi wa Jamii.


h.sep

juu sp.b
Habari Mpya  |  Kitaifa  |  Dar  |  Mikoani  |  Tahariri  |  Makala  |  Michezo  |  Matangazo  |  Webmaster
Copyright 2008 © FreeMedia Ltd.
Free media limited
mtaa wa Mkwepu na Makunganya, jengo la Bilicanas, gorofa ya kwanza, SLP 15261, Dar es salaam, Tanzania
simu +255-22-2126233  •  faksi +255-22-2126234  •  Selula  0713 296570