logo spc.r_ad0
sp.b_ad0
blu.strip
spc.bt_blu.strip
HABARI MPYA KITAIFA DAR MIKOANI TAHARIRI MAKALA MICHEZO
sp.b_menu
ban
sp.b_ban
ijumaa, 15 Februari 2008
Pekua Tovuti
sp.t_sech.box sp.tafuta_w_tuma sp.t_tuma sp.r_tuma
sp.b_box sp.b_tuma
sp.b_F1
h.sep1
sp.r_men
sp.t
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari
sp.b_tuma
sp.l_men
h.sep1
tp.spc


Wawili kushiriki marathon China


na Janelisa William


WANARIADHA wawili wa timu ya taifa ya Tanzania jana waliondoka nchini kwenda China, kushiriki mbio za Standard Chartered Marathon, zinazotarajiwa kutimua vumbi Jumapili nchini humo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Katibu Msaidizi wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), Julius Musomi, alisema kuwa chama chake kimewateua wanariadha hao wawili - Paul Sumaye na Fabiola William - ili kuiwakilisha nchi katika mbio hizo.

Musomi alisema kuwa walipata mwaliko wa kushiriki katika mashindano hayo kutoka benki hiyo, ambao ndiyo wadhamini wakuu wa mashindano hayo yanayoshirikisha mataifa mbalimbali duniani.

Naye Meneja Uhusiano wa benki hiyo, Joanitha Mramba, akizungumza katika hafla ya kuwakabidhi bendera ya taifa wanariadha hao, aliwatakia kila la heri na kuwa wanaamini wataipeperusha vema bendera ya Tanzania na kurejea na ushindi.

Mramba alisema kuwa mbali na kuwatakia mafanikio wachezaji hao, pia benki yake imetoa vifaa mbalimbali watakavyotumia wanariadha hao na gharama mbalimbali za mashindano hayo.

Alivitaja baadhi ya vifaa hivyo kuwa ni tiketi za kwenda na kurudi kwa wachezaji, suti za michezo, fulana, kofia, gharama za chakula, malazi na mahitaji mengine yatakayojitokeza katika mashindano hayo.


h.sep

juu sp.b
Habari Mpya  |  Kitaifa  |  Dar  |  Mikoani  |  Tahariri  |  Makala  |  Michezo  |  Matangazo  |  Webmaster
Copyright 2008 © FreeMedia Ltd.
Free media limited
mtaa wa Mkwepu na Makunganya, jengo la Bilicanas, gorofa ya kwanza, SLP 15261, Dar es salaam, Tanzania
simu +255-22-2126233  •  faksi +255-22-2126234  •  Selula  0713 296570