MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Ambwene Yesayah ‘AY’, amefungua kampuni ya uwakala wa wasanii wa nchi za Afrika Mashariki katika mabara ya Asia, Ulaya na Amerika.
Akizungumza na Tanzania Daima, AY amesema lengo la kuwa wakala ni kukuza na kuinua vipaji vya wasanii chipukizi na wale wenye muda mrefu katika muziki huo wa kizazi kipya katika nchi za Kenya, Tanzania na Uganda.
Aidha, kampuni hiyo itakuwa ikijishughulisha na matangazo ya biashara kwa wasanii yanayohusu masuala ya burudani.
AY anakuwa msanii wa kwanza kuwa wakala kwa lengo la kutaka kuwaendeleza wasanii wa Afrika Mashariki.
Kabla ya hapo pia msanii huyo mwishoni mwa mwaka jana alizindua mavazi yenye nembo yake.