logo spc.r_ad0
sp.b_ad0
blu.strip
spc.bt_blu.strip
HABARI MPYA KITAIFA DAR MIKOANI TAHARIRI MAKALA MICHEZO
sp.b_menu
ban
sp.b_ban
jumamosi, 16 Februari 2008
Pekua Tovuti
sp.t_sech.box sp.tafuta_w_tuma sp.t_tuma sp.r_tuma
sp.b_box sp.b_tuma
sp.b_F1
h.sep1
sp.r_men
sp.t
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari
sp.b_tuma
sp.l_men
h.sep1
tp.spc


RAAWU Chuo Kikuu wamfungulia kesi katibu wao


na Happiness Katabazi


WAFANYAKAZI 12 wa Chama Cha Wafanyakazi wa Vyuo Vikuu, Elimu ya Juu, Utafiti na Wafanyakazi Waendeshaji (RAAWU), tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), wamefungua kesi ya madai katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, dhidi ya katibu mkuu wao wa taifa.

Wafanyakazi hao wanaowakilishwa na Chistmas Swai, wanatetewa na wakili Dk. Sengondo Mvungi.

Wanaiomba mahakama iwaruhusu kufungua shauri la kufuta maamuzi ya Kamati ya Utendaji wa Taifa ya Raawu ya kuwachukulia hatua za kinidhamu viongozi wa tawi lao, kwa kusimamisha malipo ya ada za uanachama yasipelekwe taifa.

Kwa mujibu wa hati ya madai hayo, tawi la Raawu chuoni hapo lilisimamisha kupelekwa makao makuu makato ya ada za uanachama za kila mwezi kutokana na uongozi wa makao makuu kushindwa kutekeleza wajibu wao wa kutetea maslahi ya wanachama.

Wanachama hao wanalalamikia mishahara midogo na kushindwa kwa uongozi wa taifa kufanya mazungumzo na serikali kupandisha mishahara ya wafanyakazi wa chuo.

“Uongozi chuoni hapo ulifanya juhudi za kuwasiliana na viongozi wa serikali na kufanya majadiliano hayo, hivyo hawaoni kazi wanayofanya viongozi wa taifa hadi kustahili kupelekewa makato ya ada za wanachama.

Wanachama hao 12 waliopeleka hati ya maombi ya kuruhusiwa kufungua shauri la kufuta maamuzi ya uongozi wa taifa, wanapinga uamuzi wa uongozi wa taifa kuwasiliana moja kwa moja na mwajiri wao, ili kufanya mazungumzo ya kulipwa na mwajiriwa moja kwa moja badala ya kupitia akaunti ya tawi.

Wafanyakazi katika vyuo vikuu vingine kama vile Chuo Kikuu cha Afya cha Muhimbili wamekwishaanza mchakato wa kujiunga na wafanyakazi wa tawi la UDSM, jambo linaloashiria kushindwa kwa uongozi wa Raawu Taifa kukidhi matakwa ya wafanyakazi.


h.sep

juu sp.b
Habari Mpya  |  Kitaifa  |  Dar  |  Mikoani  |  Tahariri  |  Makala  |  Michezo  |  Matangazo  |  Webmaster
Copyright 2008 © FreeMedia Ltd.
Free media limited
mtaa wa Mkwepu na Makunganya, jengo la Bilicanas, gorofa ya kwanza, SLP 15261, Dar es salaam, Tanzania
simu +255-22-2126233  •  faksi +255-22-2126234  •  Selula  0713 296570