logo spc.r_ad0
sp.b_ad0
blu.strip
spc.bt_blu.strip
HABARI MPYA KITAIFA DAR MIKOANI TAHARIRI MAKALA MICHEZO
sp.b_menu
ban
sp.b_ban
jumamosi, 16 Februari 2008
Pekua Tovuti
sp.t_sech.box sp.tafuta_w_tuma sp.t_tuma sp.r_tuma
sp.b_box sp.b_tuma
sp.b_F1
h.sep1
sp.r_men
sp.t
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari
sp.b_tuma
sp.l_men
h.sep1
tp.spc


Wananchi Serengeti kuishitaki halmashauri


na Belensi Alkadi


MADHARA ya ujenzi wa hoteli za kitalii katika Hifadhi ya Taifa Serengeti bila kufanya tathimini ya uharibifu wa mazingira, yameanza kuonekana kutokana na wananchi wa Mugumu Mjini kutishia kuishitaki halmashauri hiyo, baada ya hoteli hizo kutupa taka mjini hapo.

Uamuzi wa wananchi hao wa Mtaa wa Sedeco mjini kutaka kuiburuza halmashauri mahakamani, unatokana na kukithiri kwa taka katikati ya makazi ya wananchi, zinazosababishwa na hoteli ya kitalii ya Serena, huku uongozi wa halmashauri hiyo ukiwa kimya.

 Akizungumza na Tanzania Daima, mkazi wa mtaa huo Issa Marare, alisema wanataka kuchukua uamuzi huo kutokana na malalamiko yao kwa uongozi wa halmashauri kutofanyiwa kazi.

Alisema wanaathirika na taka hizo kutokana na harufu mbaya, na pia watoto wao hucheza kwenye dampo hilo wakiokota chupa na taka mbalimbali zikiwemo kondomu.

“Tumefikia uamuzi wa kutaka kuishitaki halmashauri kutokana na kutuona sisi kama sehemu ya taka, huku wataalam wa afya wakiwa kimya, hali ambayo inatupa shaka kuwa kuna utaratibu wa maelewano baina ya wamiliki wa hoteli na wao,” alisema.

Diwani wa Kata ya Mjini, Ryoba Charles, alikiri kuwepo kwa tatizo hilo na kuwa alilikuta mwaka 2005.

Alisema amekuwa akilizungumza suala hilo katika vikao vya Baraza la Madiwani.

 Alisema Hoteli ya Serena baada ya kuona wananchi wamecharuka, wamekuwa wakimwaga taka hizo usiku.

 Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya, Dk. Maungo Kawa, naye alikiri kupokea malalamiko hayo na kusema suala hilo liko kwa mkurugenzi kwa kuwa zinahitajika fedha za kuhamisha dampo hilo.

Hoteli nyingi zilizomo ndani ya hifadhi zinadaiwa kutokuwa na maneo ya kutupa taka, hivyo kulazimika kuzitupa katika makazi ya watu.


h.sep

juu sp.b
Habari Mpya  |  Kitaifa  |  Dar  |  Mikoani  |  Tahariri  |  Makala  |  Michezo  |  Matangazo  |  Webmaster
Copyright 2008 © FreeMedia Ltd.
Free media limited
mtaa wa Mkwepu na Makunganya, jengo la Bilicanas, gorofa ya kwanza, SLP 15261, Dar es salaam, Tanzania
simu +255-22-2126233  •  faksi +255-22-2126234  •  Selula  0713 296570