logo spc.r_ad0
sp.b_ad0
blu.strip
spc.bt_blu.strip
HABARI MPYA KITAIFA DAR MIKOANI TAHARIRI MAKALA MICHEZO
sp.b_menu
ban
sp.b_ban
jumamosi, 16 Februari 2008
Pekua Tovuti
sp.t_sech.box sp.tafuta_w_tuma sp.t_tuma sp.r_tuma
sp.b_box sp.b_tuma
sp.b_F1
h.sep1
sp.r_men
sp.t
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari
sp.b_tuma
sp.l_men
h.sep1
tp.spc


Ashanti Utd yaizima Mtibwa Sugar


na Mwanne Sekuru


TIMU ya soka ya Ashanti United ya Ilala, jijini Dar es Salaam, jana ilivuna pointi tatu katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania bara iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, baada ya kuwatandika Mtibwa Sugar ya Turiani, Morogoro mabao 2-0, katika mechi iliyokuwa ya ushindani mkubwa.

Mechi hiyo, awali ilikuwa ipigwe juzi, lakini ikaahirishwa baada ya Uwanja wa Taifa, kufurika maji kutokana na mvua iliyonyesha muda mfupi kabla ya kuanza kwa mechi hiyo, hivyo kuahirishwa hadi jana ingawa timu zote zilishafika.

Ikicheza soka ya uhakika, Ashanti iliyo chini ya Kocha Ramadhan Aluko, ilikosa bao katika dakika ya 14 kwa mchezaji Bakari Kigodeko kupiga shuti fyongo na kwenda nje ya lango akiwa amebaki na kipa, Sudi Slim.

Baada ya hapo, kila timu ilifanya mashambulizi kadhaa, lakini Ashanti ndiyo ilinufaika kwa kupata bao la kwanza katika dakika ya 45, likiwekwa wavuni na Musa Kipao baada ya kufanya shambulizi kali na kudumu hadi mapumziko.

Katika kipindi cha pili, Mtibwa iliyo chini ya kocha Abdallah ‘King’ Kibadeni Mputa, ilionekana kucharuka na kufika mara kadhaa langoni mwa Ashanti, lakini umaliziaji ukawa ni tatizo.

Kama kuna mchezaji ambaye anapaswa kujilaumu katika mechi ya jana, ni kipa Slim wa Mtibwa ambaye uamuzi wake wa kutoka langoni, uliigharimu timu yake katika dakika ya 84, hivyo Adam Kingwande kufunga bao la pili kwa timu yake ya Ashanti.

Licha ya Mtibwa kufurukuta kupata walau bao la kufutia machozi, lakini vijana wa Ashanti, nao wakawa imara kuokoa hatari zote, hivyo hadi filimbi ya mwisho, Ashanti iliondoka na ushindi, hivyo kufikisha pointi 18 huku Mtibwa Sugar ikibaki na pointi 26.

Akizungumza baada ya mechi hiyo, Kibaden alikiri timu yake kuzidiwa uwezo na wapinzani wao, lakini akasema hakuna tatizo kubwa bali ni upugufu wa kawaida ambao unaweza kuondoka kwa kujipanga upya.

Aidha, alisema sababu kubwa ya kuzidiwa kwa timu yake, ni kukosekana kwa baadhi ya nyota ambao ni majeruhi na wengine kutokuwepo kikosini ambao ni Abdallah Juma, Ibrahim Mwaipopo, Kassim Juma, Meshack Abel, Monja Liseki na Abuubakar Mkangwa.


h.sep

juu sp.b
Habari Mpya  |  Kitaifa  |  Dar  |  Mikoani  |  Tahariri  |  Makala  |  Michezo  |  Matangazo  |  Webmaster
Copyright 2008 © FreeMedia Ltd.
Free media limited
mtaa wa Mkwepu na Makunganya, jengo la Bilicanas, gorofa ya kwanza, SLP 15261, Dar es salaam, Tanzania
simu +255-22-2126233  •  faksi +255-22-2126234  •  Selula  0713 296570