KATIKA hali isiyotarajiwa, watoto waliojulikana kwa jina moja moja la Yusufu na Ramadhani, wamelidanganya Kanisa la Mikocheni B Assemblies of God linaloongozwa na Mchungaji Dk. Gertrude Rwakatare, baada ya kujifanya kuwa wamedondoka kutoka angani walikokuwa wakiwanga...
MSIMU wa mvua za masika umeanza katika maeneo mbalimbali nchini, na tayari kuanza kwake kumesababisha maafa katika Jiji la Dar es Salaam na pengine katika maeneo mengine nchini. Mvua iliyonyesha Jumatano iliyopita kwa muda wa takriban saa sita hivi, imesababisha vifo vya watu watano huku madhara mengine makubwa yakitokea...
KWA akili na moyo wangu uliojaa upendo ndani ya jamii, siwezi kuwasifia wanaorudisha nyuma maendeleo ya watoto, hasa yatima ambao wanategemea msaada kwa yeyote atakayejitokeza...
SERIKALI imesema kuimarika kwa shilingi dhidi ya dola na kushuka kwa mfumuko wa bei, vimetokana na uongozi mpya wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na sera zilizowekwa na Gavana mpya Profesa Beno Ndullu....
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeshtushwa na wingi wa waandishi wa habari waliofika mkoani hapa kwa lengo la kuandika habari za kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho kinachoanza leo kijijini Butiama....
IDARA ya Uhamiaji Tanzania, imeanza kufuatilia uhalali wa vibali vya kuwawezesha kufanya kazi, wanenguaji na wanamuziki wa bendi mbalimbali hapa nchini....
TIMU ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, leo inatupa karata ya kwanza dhidi ya Harambee ya Kenya katika kuwania tiketi ya kucheza fainali mpya za Mataifa ya Afrika zitakazopigwa mwakani nchini Ivory Coast....