HABARI MPYA KITAIFA DAR MIKOANI TAHARIRI MAKALA MICHEZO
jumapili, 30 Machi 2008
Pekua Tovuti
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari


Klabu zamtaka Rage TFF


na Wilbert Molandi


KLABU 12 kati ya 14 za Ligi Kuu Tanzania Bara zimetaka aliyekuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ismail Aden Rage, kurejea katika wadhifa wake.

Kwa mujibu wa nakala iliyosainiwa na klabu hizo, klabu 12, viongozi wake wamesaini kuridhia msimamo huo, isipokuwa Yanga na Toto Africa.

Hoja ya klabu hizo 12, ni kwamba, Rage alilazimika kujiengua katika wadhifa wake kutokana na kesi iliyokuwa ikimkabili, hivyo baada ya kushinda, hana sababu ya kuwa nje.

Rage, Katibu Mkuu wa zamani wa kilichokuwa Chama cha Soka Tanzania (FAT), sasa TFF, mwaka 2005, alifungwa miaka mitatu, kwa kosa la wizi wa mali na fedha za FAT.

Hata hivyo, alikata rufaa kupinga kifungo hicho na kabla ya rufaa hiyo kusikilizwa, Desemba 2005, alitoka kwa msamaha wa Rais.

Hata hivyo, akabaki nje ya TFF kupigania rufaa yake na Alhamisi wiki hii, jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa wakiongozwa na Damian Lubuva, walimfutia makosa yaliyokuwa yamemtia hatiani Rage.

Hatua ya klabu hizo kutaka Rage arejee katika nafasi yake, imekuja siku moja tu tangu alipokaririwa akisema kuwa kama ataombwa kurejea, hatakuwa na sababu ya kukataa, ingawa angependa kupumzika.

Rage ambaye jana alikuwa miongoni mwa wajumbe wa mkutano huo wa TFF, kwa sasa ni Mkurugenzi wa timu ya Moro United.


juu

Warning: mysql_connect() [function.mysql-connect]: Can't connect to local MySQL server through socket '/var/run/mysqld/mysqld.sock' (2) in /hermes/bosweb/web098/b983/glo.freemanm2/include/comment.php on line 9
I cannot connect to the database because: Can't connect to local MySQL server through socket '/var/run/mysqld/mysqld.sock' (2)