HABARI MPYA KITAIFA DAR MIKOANI TAHARIRI MAKALA MICHEZO
jumapili, 21 septemba 2008
Pekua Tovuti
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari


Hatima ya Kaduguda Simba kujulikana leo


na Dina Ismail


MKUTANO mkuu wa wanachama wa klabu ya Simba ya Dar es Salaam unatarajia kufanyika leo kwenye ukumbi Al Muntazir, jijini. Ajenda kuu mbili zitajadiliwa.

Mwenyekiti wa Simba, Hassan Dalali alizitaja ajenda zitakazojadiliwa kuwa ni ile ya mapato na matumizi pamoja na katibu wake mkuu aliyesimamishwa - Mwina Kaduguda.

Akifafanua zaidi, ‘Field Marshal’ Dalali alisema kwamba wanachama watapata fursa ya kufahamu mapato na matumizi ya klabu hiyo, yaliyofanywa wakaguzi. Pia wanachama wataamua kama Kaduguda arejeshwe kundini ama la.

Licha ya kuwapo kwa baadhi ya watu wasioitakia mema klabu hiyo kwa kueneza uvumi wa kutofanyika mkutano wa leo, kamwe hawawezi kuivuruga klabu hiyo kwa namna yoyote ile.

“Napenda kuwahakikishia wanachama kwamba mkutano leo upo kama kawaida, hakutakuwa na vurugu wala mapinduzi kama taarifa zinavyosema…utakuwa ni mkutano wa amani kabisa,”alisema Dalali.

Mwenyekiti huyo aliongeza kwamba wanachama watakaoruhusiwa kuhudhuria mkutano huo ni wale wenye kadi mpya tu. Utoaji kadi hizo umefanyika kwa miezi kadhaa sasa.


juu

Warning: mysql_connect() [function.mysql-connect]: Can't connect to local MySQL server through socket '/var/run/mysqld/mysqld.sock' (2) in /hermes/bosweb/web098/b983/glo.freemanm2/include/comment.php on line 9
I cannot connect to the database because: Can't connect to local MySQL server through socket '/var/run/mysqld/mysqld.sock' (2)