HABARI MPYA KITAIFA DAR MIKOANI TAHARIRI MAKALA MICHEZO
jumapili, 21 septemba 2008
Pekua Tovuti
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari


Wachezaji watakiwa kujiunga NSSF


na Makuburi Ally


MAKAMU wa kwanza wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Crescentius Magori ametoa wito kwa wachezaji wa soka wa hapa nchini kuweka amana zao katika Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ili watakapostaafu soka waweze kujikimu kimaisha.

Akiwasilisha mada ya hifadhi ya jamii kwa wachezaji wa soka katika kongamano la siku tatu la makocha wa soka lililofanyika jana, katika ukumbi wa NSSF Water Front, Dar es Salaam.

Magori alisema wachezaji wengi wamekuwa wakikumbwa na tatizo la kushindwa kujikimu kimaisha baada ya soka lao kuporomoka hivyo kuwataka makocha ambao ndio walezi wa wachezaji hao kuwasaidia kimawazo wachezaji katika kukabiliana na hali hiyo.

Aidha, Magori alisema gharama za wachezaji kujiunga ni sh 10,000, lakini wachezaji wengi wamekuwa hawafanyi hivyo na kuishia kujenga heshima baa na kwa kina dada.

Magori alisema mbali ya kupata ushauri wa makocha pia nchi yetu inabidi iige mfano wa kuwa na mameneja watakaowasaidia kimawazo.

“Wachezaji inabidi wafungue miradi endelevu ya kimaendeleo na si baadaye kuanza kuomba omba kama walivyo baadhi ya wachezaji,” alisema Magori.

Kongamano hilo la siku tatu lililoanza Septemba 18 na kumalizika jana ambako lilikuwa na lengo la kujadili masuala mbalimbali kwa makocha wa soka Tanzania.


juu

Warning: mysql_connect() [function.mysql-connect]: Can't connect to local MySQL server through socket '/var/run/mysqld/mysqld.sock' (2) in /hermes/bosweb/web098/b983/glo.freemanm2/include/comment.php on line 9
I cannot connect to the database because: Can't connect to local MySQL server through socket '/var/run/mysqld/mysqld.sock' (2)