HABARI MPYA KITAIFA DAR MIKOANI TAHARIRI MAKALA MICHEZO
jumapili, 21 septemba 2008
Pekua Tovuti
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari


Kuyumba kwa Masoko ya Fedha:
Marekani inapopiga chafya, wengine itakuwaje?

 
Mwandishi Wetu


MWANZONI mwa wiki hii, mfumo wa fedha Marekani na sehemu nyingine dunaini, ulikuwa unafanana na mgonjwa aliye katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU). Hali hii ilianza zamani kidogo lakini ilijidhihirisha zaidi wakati hii.

Mfumo wa fedha unajitahidi kupambana na saratani inayosambaa. Mbaya zaidi, hakuna dalili za wazi kuwa ‘matibabu’ anayopatiwa mgonjwa huyu yana dalili za kumletea nafuu ya kudumu. Kila mara anapopewa dawa, anatulia kidogo, lakini baada ya muda, anaanza kutetema tena kwa homa.

Hiki ndicho kinachotokea katika mfumo wa fedha Marekani. Lakini athari zake zinaonekana kusambaa dunia nzima. Maeneo ambayo masuala ya masoko ya efdha yanachukua nafasi kubwa, athari hizi zimeshaanza kuonekana wazi wazi. Masoko ya hisa katika nxchi za Ulaya na Asia, yameshaonesha kutikisika. Afrika pekee, bado haijaelezaa, au haijaelezewa inathirika vipi kutokana na mtikisiko huu unaoikumba Marekani hivi sasa.

Lakini ni dhahiri kuwa Afrika nayo inaathirika kwa sababu mifumo ya kiuchumi ya nchi nyingi, kana si zote barani humu, ni tegemezi kwa Ulaya au Marekani. Hivyo, ni dhahiri kuwa wakati huu Marekani na Ulaya zitakapokuwa zinapiga chafya kutokana na kupaliwa na matatizo ya kiuchumi, nchi za Afrika zitakuwa katika hali mbaya sana ingawa hilo linaweza lisionekne katika kipindi hiki.

Mgonjwa huyu amewatia kiwewe madaktari ambao sasa wanaonekana nhawajui wafanye nini kuokoa maisha yake. Katika kuhangaika kwao, madaktari wanajaribu hata mbinu nyingine ambazo hawakupata kuzijaribu awali.

Na hali hii inaonekana si kutisha, bali imewachosha watu wanaotakiwa kuhakikisha kuwa uchumi unakwenda sawasawa. Mapema wiki hii, maofisa wa taasisi za fedha Marekani, walionekana kuwa wachovu kupita kiasi wakati walipokutana na vionmgozi wa Congress, kuwapa taarifa kuhusiana na hatua ambazo serikali imezichukua kuiokoa kampuni ya bima ya AIG.

Lakini pamoja na uchovu wao, maofisa hao wa Benki Kuu na Hazina ya Marekani wanaonekana kuwa wameshautambua ugonjwa huo. Wanasema matatizo ya mfumo wa fedha yanayoonekana sasa yanatokana na mkusanyiko wa madeni.

Wakati taasisi zilipotoa mikopo kwa wingi, wau binafsi na taasisi zilichukua mikopo mikubwa na mingi. Kati ya mwaka 2002 na 2006, ukopaji miongoni mwa Wamarekani ulikua kwa wastani wa asilimia 11 kwa mwaka, kiwango ambacho ni kukibwa sana ikilinganishwa na kukua kwa uchumi.

Ukopaji wa taasisi kubwa nao ulikuwa kwa wastani wa asilimia 10 kwa mwaka. Hivi sasa, wengi wa wakopaji hawa hawawezi kulipa mikopo yao, suala ambalo linafanywa kuwa gumu zaidi na kushuka kwa bei ya nyumba. Kutokana na hali hii, watu wengi wengine wanaogopa kukopa zaidi wakihofia kufikwa na hali mbaya inayowakuta wakopaji wengine hivi sasa. Hali hii inatishia sana kuyumbisha uchumi kwa kiasi kikubwa.

Kuna mambo kama matatu yanayoweza kukomesha hali hii ya mikopo isiyo ya kawaida, na yanatakiwa yafanyike haraka. Taasisi za fedha zinapaswa kusamehe madeni yasiyolipika, kuachia au kuuza dhamana walizonunua kutokana na fedha walizokopa. Pili, wanapaswa kulipa madeni yote wanayodaiwa. Tatu, wanapaswa kujenga mfumo ambao utawakinga dhidi ya matukio ya aina hii. Wanatakiwa kuwa na mfumo ambao utahakikisha kuwa fedha zao na madeni yao yapo salama siku zote.

Lakini tatizo linalojitokeza ni kuwa ni vigumu kupata thamani halisi ya nyingi ya dhamana zilizopo hivi sasa. Hii ni kwa sababu vitu vingi vilivyowekwa dhamana vimepoteza thamani yake halisi kutokana na matatizo katika mifumo ya fedha.

Kujaribu kuuza dhamana hizo kwa wingi kunashusha zaidi bei yake katika soko na hivyo kufanya iwe vigumu kuziuza kwa faida inayotakiwa. Lakini hii inazisukuma taasisi nyingi kuingiza dhamana sokoni kwa lengo la kutafuta fedha zinazohitajika sana hivi sasa ili kuziokoa zisife.

Hali hii inazidi kushusha thamani ya hisa za taasisi na kampuni hizo. Inakuwa vigumu kwao kuzidi kukusanya fedha kupitia mauzo ya hisa kwa sababi hisa nazo zinashuka thamani kwa kuwa watu wengi wanataka kuuza ili kujiondoa katika hali ya kupata hasara.

Wanaogopa kukopa

Hali ya kukua kwa mikopo kuliko uchumi ilianza kushika kasi mwaka 2006. awali, hali hii ilikuwa inaonekana katika sehemu chacvhe duniani. Lakini sasa imesambaa katika nchi nyingi. Hali hii imeathiri mikopo ya muda mfupi, kama vile ya nyumba na ujenzi, ambayo mabenki wanaitumia sana kuongeza faida zao.

Katika robo ya kwanza na mwaka, taasisi za fedha zimepunguza kukopa kwa asilimia 5.1, kiwango ambacho ni nusu ya wastani wa kati ya mwaka 2002 na 2007. mbaya zaidi, mikopo kwa ajili ya nyumba nayo imepungua sana hadi kwenye wastani wa asilimia 3.5.

Mchumi wa Goldman Sachs Group Inc., Jan Hatzius, anakadiria kuwa mwaka jana pekee, taasisi za fedha duniani kote zilifuta mikopo ya dhamana zenye thamani ya dola bilioni 408, lakini taasisi hizo zikafanikiwa kukusanya dola bilioni 367 katika mitaji yao.

Lakini hii inaonekana kuwa haisaidii. Kila mara mabenki na taasisi zinazokopesha zinapotangaza kuwa zimesamehe madeni na kukusanya mitaji zaidi, ndipo wimbi la uthaminishaji upya wa dhamana. Hii huanzisha upya tatizo lile lile.

Inakadiriwa kuwa hasara kutokana na dhamana zisizouzika itafikia dola bilioni 636 mwaka 2012. Hii itasababisha benki nyingi sana zipunguze kiwango cha mikopo kinacvhotolewa. Watalaamu wanasema ili kukabiliana na hali hiyo, mabenki yatapaswa kuounguza mikopo kwa wastani wa silimia 1.8 kwa mwaka ili kulingana na ukuaji wa uchumi kati ya mwaka huu na mwanai. Hii ni sawa na kupoteza dola bilioni 250 kila mwaka.

Tatizo jingine linaloweza kujitokeza ni watu wanaotumia mikopo kuendesha shughuli zao. Katika kipindi hiki ambacho mabenki yapo katika mbinyo, wakopaji hawa hawataweza tena kukopa. Baadhi ya wawekezaji, hasa katika sekta ya fedha, wanaanza kuangalia matatizo yao wenyewe wakati watu wa taasisi za fedha wakishughulika na matatizo yao. Wengi wa wawekezaji hawa walikopa fedha kuwekeza na sasa wanapata shida kukopa fedha zaidi kwa ajili ya kuendeleza miradi yao.

Misukosuko ya mifumo ya fedha inayotokana na mikopo ina historia ndefu huko Marekani. Tangu wakati wa kile kinachonmjulikana kama Depression, hadi matatizo ya masoko ya fedha ya nchi za Asia katika miaka ya 1990. wachumi na watengeneza sera inaonekana wamekosa jibu la haraka na la uhakika la matatizo haya kwa sababu bado yanaendelea kujirudiarudia kwa miaka.

Hadi sasa, suluhu zilizopatikana, kama vile kushusha riba na kusamehe madeni, zinaonekana kutuliza tu na si tutibu tatizo hili. Wakati mwingine hatua hizi zinachelewesha tu tatizo.

Katika mazingira kama haya, viongozi wanajaribu mbinu na njia mbalimbali kukabili tatizo hili. Franklin Delano Roosevelt kwa mfano, alianzisha taasisi na kutunga taratibu mpya baada ya kuyumba kwa masoko mwaka 1929. katika miaka ya 1990, Japan japan ilijikuta ikifanya matumizi yasiyohitajika bila kutarajia kutokana na matatizo kama haya haya.

Rais George H.W. Bush na Congress waliunda taasisi maalum kwa ajili ya kushughulikia mashirika yaliyoanguka kutokana na matatizo ya aina hii. Huko Hong Kong, mwaka 1998, serikali iliamua kununua hisa za kampuni ambazo zilikuwa zinakufa kutokana na mjatatizo ya aina hii ambazo zilikuwa zimeandikishwa katika soko la hisa la Hang Seng.

Leo serikali zimeamua kutoa fedha kwa benki zake kuu ili kuokoa hali ya mambo. Wiki hii, serikali zipatazo sita zimechukua hatua hii ili kuyaokoa mashirika na makampuni ambayo iwapo yataanguka, madhara yake yatakuwa makubwa kwa serikali, mashirika, makampuni, taasisi na hata kwa watu binafsi na wanasiasa.

Lakini yapo makampuni na taasisi zinazofikiria kuungana. Mfano mzuri ni ule wa Merrill Lynch & Co kuuza sehemu yake kwa Bank of America Corp. Itakumbukwa kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, katika harakati za kujinasua, Merrill iliajiri Ofisa Mtendaji Mkuu mpya, ikafuta madeni mabaya yanayofikia thamani ya dola bilioni 41.4 na kufanikiwa kukusanya mtaji wa dola bilioni 21.

Lakini haikuweza kuhimili msukosuko wa sasa. Kila jinsi ilivyokuwa inajitutuma, ndivyo ilivyokuwa inalazimika kufuta madeni zaidi.

Akiangalia benki kubwa kama Lehman Brothers ikianguka, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Merrill, John Thain, alisema kuwa alifahamu wao ndio wanaofuatia katika anguko hilo.

Katika nyakati za kawaida, kampuni zinapokumbwa na matatizo kama haya huweza kujitafutia fedha kutoka vyanzo vingine na kuendelea na shughuli zake kama kawaida. Lakini kila taasisi inapotishiwa na hali hii, unakimbilia wapi?

Awali, kama ilivyo kawaida ya wafanyabiashara, ilidhaniwa kuwa hasara hii inaweza kutupwa kwa walaji. Lakini huko Marekani huu ni mwaka wa uchaguzi na wanasiasa wanashindana kuwahakikishia wananchi maisha bora. Haingekuwa busara kwao wao kuwatupia wananchi hasara hii, hasa katika kipindi hiki cha kampeni.

Ndiyo maana lilitolewa pendekezo kuwa ianzishwe taaisi maalum itakayoshughulikia taasisi za fedha zote zote zitakazoanguka kutokana na kuanguka kwa masoko ya fedha.

Lakini mtaalamu mwingine wa masuala ya fedha, William Seidman, ana wazo jingine. “Inapotokea hasara kubwa kama hii, kuna watu watatu tu ambao wanaweza kuichukua hasara hiyo. Watu wanaomiliki dhamana, wenye hisa na serikali. Huo ndio mchezo tunaoucheza hivi sasa. Hivi kweli tunawezza kuirusha hasara hii kwa walipa kodi?”

Hata vwanasiasa ambao wapo kwenye kampeni nao wameonyesha jitihada za kutafuta njia mbadala ya kuhakikisha kuwa hasara hii haipelekwi kwa mwananchi wa kawaida.

Ili kuonyesha dhamira yake, juzi baraza la Congress lilitangaza liliahidi hatua za haraka sana kununua dhamana zote ambazo zimeingia matatizoni, zinazoshikiliwa na benki ambazo zipo katika msukosuko. Hatua hii inalenga kuhakikisha kuwa hali ya mambo katika masoko ya fedha inatengemaa.

Waziri wa fedha wa Marekani, Henry Paulson, na mwenyekiti wa benki Kuu, Ben Bernanke, inaelezwa kuwa wapo wakibuni mbinu mopya za kukabiliana na hali hii na kupendekeza kwa watunga sheria hao ili waipitishe rasmi na kuanza kutumika.

“Tutaifanyia kazi haraka sana, hatuna muda wa kutosha,” alisema spika wa baraza hilo, Nancy Pelosi.

Lakini kuna jambo la kushangaza katika smukosuko huu. Watu wanashangaa ni kwa nini matatizo yote haya, licha ya kuleta taharuki kubwa, lakini madhara yake si makubwa sana katika uchumi! Hata kiwango cha ukosefu wa kazi kipo katika asilimia 6.1, hata hakijakaribia kiwango cha hatari cha asilimia 7.8 kilichorekodiwa mwaka 1992 yalipotokea matatizo kama haya.

Hii inaweza kuwa ni kwa sababu serikali imechukua hatua haraka. Great Depression iliuumiza sana uchumi kwa sababu serikali ilichukua hatua za udhibiti zaidi na kuharibu kila kitu.

Lakini hatua za hivi majuzi, kwa mfano kwa serikali ya Marekani kukubali kuikoa kamopuni ya bima ya AIG, na serikali nyingine kutoa fedha kupitia benki zao kuu, kumesaidia kurejesha imkani ya wanahisa na wawekezaji kuwa hali ya mambo haityokuwa ngumu. Ndiyo maana baadhi ya masoko ya hisa ulimwenguni yameanza kurejea katika hali yake ya kawaida.

Aidha, uchumi, ambao umepanuka sana na kuzidi kuimarika, wenyewe ndio umeweza kuhimili hali hii. Uuzaji nje umeimarika na uchumi sehemu nyingine duniani haujaathirika sana kiasi cha kuwafanya washindwe kuendelea kuagiza bidhaa kutoka Marekani na nchi nyingine.

Nchi zenye uchumi imara namna hivyi zinaweza kuwa hazijaathirika kiuchumi, lakini je, nchi nyingine zenye uchumi tegemezi, kama nchi nyingi za Afrika, zinaweza kuathirika na hali hii? Hii ni dhahiri kwa sababu sehemu kubwa ya bajeti za nchi tegemezi hutoka kwa nchi hizo kubwa. Kutokana na matatizo haya, nchi kubwa zinalazimika kutenga fedha nyingi za dharura ili kuziokoa taasisi zao. Kwa maana hiyo, upo uwezekano wa wao kupunguza au hata kuchelewesha miasaada yao kwa nchi zinazoendelea.

Ni dhahiri kwua wanapopiga chafya, sisi huku tunaweza kuwa tunapatwa na mafua kabisa.


juu

Warning: mysql_connect() [function.mysql-connect]: Can't connect to local MySQL server through socket '/var/run/mysqld/mysqld.sock' (2) in /hermes/bosweb/web098/b983/glo.freemanm2/include/comment.php on line 9
I cannot connect to the database because: Can't connect to local MySQL server through socket '/var/run/mysqld/mysqld.sock' (2)