HABARI MPYA KITAIFA DAR MIKOANI TAHARIRI MAKALA MICHEZO
jumatatu, 22 septemba 2008
Pekua Tovuti
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari


Waliowashambulia maofisa TANAPA kortini leo


na Ramadhani Siwayombe, Arusha


WANAKIJIJI 17 kutoka Kijiji cha Nasura, wilayani Arumeru, Arusha. waliokamatwa wiki moja iliyopita kwa tuhuma za kuwashambulia askari wa TANAPA wanafikishwa mahakamani leo.

Kufikishwa mahakamani kwa wanakijiji hao kunatokana na malalamiko ya ndugu wa wanakijiji hao kwa Jeshi la Polisi kuwanyima dhamana ndugu zao na kuendelea kuwaweka rumande kwa muda mrefu.

Akizungumza na Tanzania Daima jana kuhusiana na malalamiko hayo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Basilio Matei, alisema hali ya kukaa rumande kwa muda mrefu kwa wanakijiji hao imetokana na kuchelewa kuandaliwa kwa mashitaka yao na wanasheria wa serikali.“Ndugu yangu unajua hivi sasa baada ya sisi kukamata wahalifu kuna wanasheria wa serikali ndio wamepewa kazi ya kuandaa mashtaka kwa watuhumiwa kwa ajili ya kupeleka mahakamani, hivyo hao ndio wanachelewesha kuandaa mashitaka na kusababaisha hali hiyo kujitokeza,” alisema kamanda Matei.

Alisema baada ya kukaa kwa muda huo, juzi ndio mashtaka yao yalikuwa tayari na hivyo kushindwa kuwaachia kwa kuwa ni wengi kuepuka wengine kutotokea muda muafaka wakati wa kupelekwa mahakamani.

Wanakijiji hao ni miongoni mwa wanakijiji 31 waliokamatwa na kuwekwa ndani ambapo kati yao 14 waliachiwa kwa sababu mbalimbali ikiwemo uzee na kubaki hao 17 ambao wanakabiliwa na mashitaka ya kushambulia maofisa wa hifadhi.

Wananchi hao wa kijiji cha Nasura, Kata ya Engarenanyukii waliwashambulia maofisa wa hifadhi ya TANAPA, Septemba 11 mwaka huu ambao walikuwa kazini katika doria za kawaida.

Ilidaiwa chanzo cha vurugu hizo ni baada ya maofisa hao kufika katika kijiji hicho na kukuta kinamama watatu wakikata miti ndani ya msitu wa hifadhi hiyo.

Baada ya kuwakuta waliwafuata kwa lengo la kuwakamata ndipo kinamama hao walipopiga mayowe na wanakijiji walifurika eneo hilo na kuanza kuwashambulia maofisa hao.


juu

Warning: mysql_connect() [function.mysql-connect]: Can't connect to local MySQL server through socket '/var/run/mysqld/mysqld.sock' (2) in /hermes/bosweb/web098/b983/glo.freemanm2/include/comment.php on line 9
I cannot connect to the database because: Can't connect to local MySQL server through socket '/var/run/mysqld/mysqld.sock' (2)