HABARI MPYA KITAIFA DAR MIKOANI TAHARIRI MAKALA MICHEZO
jumatatu, 22 septemba 2008
Pekua Tovuti
Gazeti la Jana
Matangazo
Bei zetu
Wasiliana nasi
Tuma habari


Vodacom yaanika chipukizi 40


na Dina Ismail


KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom jana ilitangaza majina 40 ya chipukizi watakaoingia katika kambi maalum ya Vodacom Global Soccer Star Academy (VGSS) watakaoingia kambini kesho katika hoteli ya National iliyopo Chang’ombe jijini Dar es Salaam.

Meneja udhamini wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, Emillian Rwejuna alisema, wakiwa katika kambi hiyo itakayodumu kwa muda wa wiki tano, wanasoka hao watakuwa wakijifunza mambo mbalimbali yahusuyo soka na afya.

Alisema kila wiki watakuwa wakitolewa wachezaji wawili kabla ya kubaki wawili ambako mmoja atapata nafasi ya kwenda kuichezea klabu ya Reading ya Uingereza wakati mwingine atapata nafasi ya kwenda kusoma katika chuo cha Nabera Soccer Academy kilichopo, Hispania.

Naye Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Sunday Kayuni alisema vigezo vilivyotumika kuwapata nyota hao ni pamoja na kuwa na maumbile yanayokubalika kisoka ikiwemo nguvu, kasi na stamina.

Kigezo kingine ni kumiliki mpira na ugawaji wake, ufahamu wa mchezo sanjari na kutafuta nafasi ya kucheza pasi ambazo zinasaidia kufungua vyumba kwa timu.

“Kigezo kingine ni kucheza kwa kujituma, kutafuta nafasi za kupeleka mpira mbele na kufungua na kutafuta nafasi za kushambulia, pia kuripoti kambini kwa wakati stahili,” alisema Kayuni.

Wachezaji hao ni pamoja na Hamisi Mroki, Gossage Ally, Athumani Kibige, Imran Omary (Arusha), Robert Joseph, Hassan Bakari, Edger Alexander, Emmanuel Mkumbo, Aman Juma, Ibrahim Job, Maengo Hitemu, Mohamed Athuman (Mwanza).

Pia wamo Francis Casto, Halfan Ngecha, Shadrack Emmanuel, Daniel Kasekenya, Sannu Essau, Cosmas Mwazembe, Jimmy Shoji, Emmanuel Manka (Mbeya), Aboubakar Ally Abdullah, Salum Bakari Sad, Hussein Ramadhan Kisunzi, Nassor Ally Omar, Wazir Ramadhan Suleiman, Abdallah Rashid Abdallah (Zanzibar).

Wengine ni Athumani Said, Peter Oswin Nungu, Shaban Maulid Chande, John Andrea Msagati, Hassan Shaban Jabu, Shukuru Ally Mangula, Habib Maulid Mtumbuka, Gideon Daudi Sepo, Atupele Green Jackson, Daud Gabriel Mwasongwe, Hamis Seif, Alex Athanas Thomas na Salum Salum Mzange (Dar es Salaam).


juu

Warning: mysql_connect() [function.mysql-connect]: Can't connect to local MySQL server through socket '/var/run/mysqld/mysqld.sock' (2) in /hermes/bosweb/web098/b983/glo.freemanm2/include/comment.php on line 9
I cannot connect to the database because: Can't connect to local MySQL server through socket '/var/run/mysqld/mysqld.sock' (2)