HABARI MPYA LA JANA MATANGAZO BEI ZETU WASILIANA NASI TUMA HABARI
jumanne, 27 julai 2010
Yaliyopita
Pekua Tovuti

Dereva teksi mbaroni kwa wizi


na Muhiba Haji

 

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limemkamata dereva teksi, Mohamed Amiri kwa tuhuma za kuhusika na wizi uliotokea katika Hoteli ya Kilimanjaro ‘Kempiski’, Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Charles Kenyela, alisema jana kuwa wizi huo ulitokea juzi majira ya saa 10 alfajiri katika hoteli hiyo, ambapo Mkurugenzi wa hoteli hiyo raia wa Uingereza, Hasmukh Masrani (61) aligundua kuibiwa chumbani mwake.

Kenyela alisema miongoni mwa mali zilizoibiwa ni simu nane, dola 3,000 za Marekani, euro 2000, leseni mbili za udereva ya Tanzania na Uingereza, tiketi mbalimbali za ndege pamoja na nguo aina mbalimbali za kiofisi.

Alisema jirani na chumbani kwa Masrani kulikuwapo na mpangaji, Peter Masumbo, mfanyakazi wa Kampuni ya Predage Tanzania Mineral Investment Ltd ya jijini Dar es Salaam ambaye alitoroka baada ya tukio hilo.

Hata hivyo Kenyela alisema dereva huyo alikataa kuhusika na tukio hilo bali alipewa baadhi ya nyaraka kuzipeleka katika hoteli hiyo bila ya kujua zinahusiana na nini.



juu