KOZI ya Kujenga Afya inayoratibiwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa
(Fifa) ‘FIFA 11 for Health,’ imeanza jana kwenye Ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ikishirikisha walimu 18 wa shule za msingi na makocha 12
wa soka.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, kozi hiyo ni mpango wa Fifa kwa ajili ya kujenga afya kupitia mchezo huo unaopendwa na watu wengi kote ulimwenguni.
“Kozi hiyo ya siku tano inayoitwa ‘Fifa 11 for Health’ imeanza leo
(jana) na itamalizika Juni 15,” alisema Wambura.
Wambura alisema mafunzo hayo yanayoendeshwa na wakufunzi kutoka
Fifa, yatakwenda na ujumbe mbalimbali kwa wachezaji na mashabiki kama
‘Cheza Mpira’, ‘Heshimu Wasichana na Wanawake’.
Nyingine ni ‘Jikinge na Virusi vya Ukimwi (HIV)’, Epuka Dawa za Kulevya, Pombe na Sigara’, ‘Tumia Neti Zenye Viuatilifu, Nawa Mikono Yako, Kunywa Maji Salama, Kula Chakula Chenye Mpangilio, Pata Chanjo, Tumia Dawa Sahihi na Cheza Mchezo Mzuri’.
Aliwataja Walimu kutoka shule za Dar es Salaam kuwa ni Aloyce Rutta (Montfort, Temeke), David Kazinge (Temeke, Temeke), Rajabu Ased (Mtoni Kijichi, Temeke) na Mathew Kambona (Mji Mwema, Temeke).
Wengine ni Ruth Mahenge (Chang’ombe, Temeke), Abdul Mikoroti (Nzasa, Temeke), Exuperus Kisaka (Mavurunza, Ilala), Khadija Kambi (Karume, Ilala) na Hamisi Ibrahim (Tusiime, Ilala).
Wamo pia Baltazar Kagimbo (Tabata Jica, Ilala), Isaac Mhanza (Airwing, Ilala), Baraka Baltazar (Muhimbili, Ilala), Job Ndugusa (Upanga, Ilala) na Tumaini Hiluka (Buguruni, Ilala).
Maua Rashid (Uhuru Wasichana, Ilala), Mussa Kapama (Bunju A, Kinondoni), Raymond Rupia (St. Anne Maria, Kinondoni) na Priscus Shilayo (JK Nyerere, Kinondoni).
Makocha ni Dismas Haonga, Frank Mwakang’ata, John Sebabili, Michael Bundala, Peter Manyika, Raphael Matola, Renatus Magolanga, Robert Mayunga, Saidi Pambaleo, Seba Nkoma Titus Michael na Wilfred Kidao.
Wambura alisema, programu hiyo inalenga watoto na kusema washiriki watakaofaulu, watakuwa wakufunzi kwa ajili ya kuitekeleza kwenye maeneo mbalimbali nchini.
Katika hatua nyingine, waamuzi 54 wanashiriki kozi inayotambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), iliyoanza jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambayo itafungwa Juni 14.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
Boniface Wambura, kozi hiyo inaendeshwa na wakufunzi wawili kutoka
Fifa, wakisaidiwa na wakufunzi wanne wa Tanzania.
Wakufunzi wa Fifa ni Carlos Henriques na Mark Mizengo na wazawa,
ni Kapteni mstaafu Stanley Lugenge, Leslie Liunda, Soud Abdi na Riziki Majala