HABARI MPYA LA JANA MATANGAZO BEI ZETU WASILIANA NASI TUMA HABARI
jumamosi, 16 juni 2012
Yaliyopita
Pekua Tovuti

Jela miaka 20 kwa kuua pundamilia


na Ahmed Makongo, Bunda

 

WATU watatu wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kila mmoja na Mahakama ya Wilaya ya Bunda, mkoani Mara baada ya kupatikana na hatia ya kuua pundamilia ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kinyume cha sheria.

Hakimu Mkazi Mwandamizi, Joackim Tiganga alisema jana kuwa ametoa adhabu hiyo baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka mahakamani hapo.

Hakimu Tiganga, alisema ametoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwao na kwa watu wengine wenye tabia na nia ya kuwinda wanyama kinyume cha sheria.

Waliohukumiwa kiungo hicho ni Joseph Lazaro, Inocent Amos na Emmanuel Juma, wote wakazi wa Kijiji cha Kunzugu, wilayani hapa.

Awali, Mwendesha Mashitaka wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Mwanasheria Emmanuel Zumba, alidai washitakiwa hao walikamatwa na askari wa hifadhi hiyo, wakiwa wanawinda wanyama kwa kuwafukuza na pikipiki, na kisha kuwashambulia kwa silaha za jadi.

Alidai washitakiwa wote walikamatwa wakiwa wameshaua pundamilia mmoja mwenye thamani ya sh 510,000.



juu