HABARI MPYA LA JANA MATANGAZO BEI ZETU WASILIANA NASI TUMA HABARI
jumamosi, 16 juni 2012
Yaliyopita
Pekua Tovuti

Serikali yaagiza nyumba kurejeshwa


na Happiness Mtweve, Dodoma

 

SERIKALI imeagiza kurejeshwa kwa nyumba za maendeleo ya jamii (Community Center) zilizopo nchini ambazo zilikuwa zikitumika kutoa mafunzo mbalimbali, ambazo hivi sasa zinatumika kama ofisi.

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu, alitoa kauli hiyo mjini hapa jana alipozungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yanayoadhimishwa Juni 16 kila mwaka.

Alisema awali nyumba hizo zilijengwa na serikali kwa ajili ya kutoa elimu za kijamii kwa wanawake na watoto, lakini hivi sasa zimebadilishwa na kufanyiwa kazi ambayo haikukusudiwa.

“Kuna baadhi ya mikoa ambayo ina nyumba za maendeleo (Comumunity Centers), lakini hivi sasa zimegeuzwa ofisi kinyume na malengo ya serikali,” alisema.

Hata hivyo, alisema serikali itahakikisha inajenga majengo mapya katika mikoa ambayo nyumba hizo hazikujengwa, ili kusaidia watoto na wanawake kupata mafundisho mbalimbali ya kijamii.



juu