HABARI MPYA LA JANA MATANGAZO BEI ZETU WASILIANA NASI TUMA HABARI
jumamosi, 30 juni 2012
Yaliyopita
Pekua Tovuti

Super D kugawa ujuzi Kilombero


na Salum Mkandemba

 

KOCHA wa mchezo wa masumbwi hapa nchini, Rajabu Mhamila 'Super D' anajipanga kuitumia vema fursa ya mwaliko wa kwenda kufundisha na kuwapatia ujuzi mabondia na makocha wa klabu ya Kilombero Boxing ya Ifakara alioupata hivi karibuni.

Akizungumza na gazeti hili jana, Super D alisema, amemejipanga kuwanufaisha wote watakaoahudhuria mafunzo yake, aliyoyapata kutoka kwa mwenyekiti wa klabu hiyo Hiyari Bohari na Katibu wake Ramadhan Mindu, kwa siku mbili hapo Agosti mwaka huu.

Aliongeza kuwa mwaliko huo unalenga kuwanoa makocha na kuwapatia ujuzi wa ziada mabondia chipukizi walioko katika klabu hiyo, na wakali wengine walioko mkoani Morogoro, hususan wilaya ya Kilombero.

“Nimevutiwa na mwaliko huu na sasa najipanga kuwapa makali washiriki. Natoa mwito kwa wakazi wa Ifakara na Kilombero kwa ujumla kujitokeza kwa wingi, ili kuvuna kilicho bora katika masumbwi,” alisema Super D.

Aidha, Super D aliongeza kuwa, mchezo wa masumbwi ni miongoni mwa michezo pendwa nchini, ingawa anashangaa kuona unakosa wafadhili kwa ajili ya kutoa sapoti mbali mbali.

Akatumia fursa hiyo kuwataka wafadhili kutoka makampuni mbalimbali ya umma na ya serikali pamoja na wadau wa michezo kujitokeza kusaidia kwa namna moja au nyingine hususan mafunzo anayotaka kuyatoa akiwa Kilombero.



juu