HABARI MPYA LA JANA MATANGAZO BEI ZETU WASILIANA NASI TUMA HABARI
jumatano, 4 julai 2012
Yaliyopita
Pekua Tovuti

Miradi ya maji Mbeya kugharimu bil. 1/-

JIBU LA SWALI LA MBUNGE Mbeya vijijini

na Mwandishi wetu, Dodoma

 

MIRADI mitatu ya maji katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya Vijiji itagharimu kiasi cha sh. bilioni 1.1 bunge limelezwa.

Hayo yalielezwa Bungeni jana na Naibu Waziri wa Maji, Dk. Binrithi Mahenge wakati akijibu swali la Mch. Luckson Mwajale.

Katika Swali hilo mbunge lilitaka kujua ni lini maji yataanza kusambazwa katika vijiji vyake mbali na serikali kuahidi kusambaza maji katika vijiji hivyo toka bunge lililopita.

Akijibu swali hilo Naibu huyo alisema halmashauri ya wilaya ya Mbeya vijijini inatekeleza programu ya maji na usafi wa mazingira vijiji kwenye vijiji 17 vya kipaumbele ilivyochagua.

“Serikali inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali hapa nchini lengo likiwa kuhakikisha wananchi katika maeneo mengi wanafikiwa na huduma hiyo,” alisema Mahenge.

Alisema kuwa kwa awamu ya kwanza utekelezaji utahusisha vijiji vitatu vya Shongo, Igale na Iwalanje ambavyo tayari mkandarasi wa ujenzi wa miundombinu amepatikana na ujenzi utaanza na kukamilika katika mwaka huu wa fedha wa 2012/2013.

Alielza kuwa miradi hiyo itagharimu jumla ya sh bilioni 1.1 fedha ambazo zitatumika katika vijiji ambavyo vimepewa kipaumbele.



juu