HABARI MPYA LA JANA MATANGAZO BEI ZETU WASILIANA NASI TUMA HABARI
jumatano, 4 julai 2012
Yaliyopita
Pekua Tovuti

Banda la Kanumba kivutio Sabasaba


na Nasra Abdallah

 

BANDA la maonesho la Msanii nguli, marehemu Steven Kanumba ‘The Great’ lililoko viwanja vya maonesho ya Mwalimu Nyerere, ‘Sabasaba’ Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam, limekuwa kivutio kikubwa cha watazamaji wanaofika katika maonesho hayo.

Katika banda hilo, bidhaa mbalimbali zenye picha za Kanumba zinauzwa ikiwemo kalamu, fulana, vikombe, vitunza funguo, ‘Key holder’ na ‘frame’ za kuwekea picha na filamu ambazo aliigiza tangu hajaanza kumiliki kampuni yake.

Mbali na vifaa hivyo, pia kuna mavazi mbalimbali ambayo Kanumba alikuwa akipenda kuyavaa enzi za uhai wake, kama vile viatu, kofia na suti.

Pia mama yake Kanumba, amekuwepo katika banda hilo kwa ajili ya kujibu maswali mbalimbali kutoka kwa mashabiki wa msanii huyo.

Msanii huyo nguli, alifariki dunia Aprili mwaka huu, baada ya kutokea ugomvi kati yake na mpenzi wake ambaye pia ni msanii wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu.’



juu