HABARI MPYA LA JANA MATANGAZO BEI ZETU WASILIANA NASI TUMA HABARI
jumatano, 4 julai 2012
Yaliyopita
Pekua Tovuti

Magharibi yaanza vema soka UMITASHUMTA


na Clescencia Tryphone

 

KANDA ya Magharibi imeanza vema michuano ya Shule za Msingi (UMITASHUMTA), kwa upande wa soka maalumu (wasiosikia), baada ya kuwapiga Nyanda za Juu mabao 5-0.

Magharibi, ilionekana kutawala takriban dakika zote za mchezo huku Nyanda za Juu wakionekana kukata tamaa mara baada ya kubugizwa mabao hayo.

Mbali na soka maalumu, katika soka ya kawaida, Dar es Salaam nao walianza vema kwa kuwachapa Magharibi kwa mabao 2-1.

Wavu Nyanda za Juu Kusini waliwafunga Magharibi kwa seti 2-1, huku Nyanda za Juu wakilala seti 3-2 dhidi ya Dar es Salaam.

Kwenye mikono, Magharibi wasichana waliifunga bila huruma Kaskazini Mashariki kwa magoli 10-1, huku Rose Gerald aking’ara kwa kutupia magoli manne peke yake.

Michuano hiyo inaendelea tena leo katika viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha, Pwani na inatarajiwa kufika tamati Julai 11, mwaka huu.



juu