HABARI MPYA LA JANA MATANGAZO BEI ZETU WASILIANA NASI TUMA HABARI
jumanne, 10 julai 2012
Yaliyopita
Pekua Tovuti

Watishia kususia sensa


na Happiness Mnale, Mkuranga

 

WAKULIMA wa zao la korosho wilayani Mkuranga, mkoa wa Pwani wameitaka serikali kuwalipa fedha zao za mauzo ya zao hilo kwa msimu wa kilimo 2011/2012, vinginevyo watasusia sensa itakayoanza Agosti 26 mwaka huu.

Walidai kuwa bila kulipwa watahakikisha wanafunga shule zote za msingi na sekondari na kuamua nguvu ya umma ifanye maandamano hadi ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo.

Akizungumza jana jijini Dar es Salam, mwakilishi wa wakulima hao, Ramadhani Gugwe, alisema kuwa pamoja na Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kutoa tamko la kuhakikisha wanalipwa lakini wanashangazwa ni kwa nini hawalipwi wala kuelezwa lini fedha zao zitaingizwa benki.

Gugwe alisema kuwa wanashangazwa na viongozi wa wilaya hiyo ambao wanaendekeza ukiritimba na ufisadi katika kuwalipa fedha huku wenzao wa Mtwara wakilipwa fedha zao.



juu