HABARI MPYA LA JANA MATANGAZO BEI ZETU WASILIANA NASI TUMA HABARI
jumanne, 10 julai 2012
Yaliyopita
Pekua Tovuti

Ubora wa vitunguu vya Singida watambuliwa

JIBU LA SWALI LA MBUNGE Viti Maalum

na Mwandishi wetu, Dodoma

 

NAIBU Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam Malima, amesema kuwa serikali inatambua kuwa vitunguu vinavyozalishwa katika Wilaya mpya ya Mkalama, mkoani Singida vina ubora ndani ya nchi za Afrika Mashariki na Kati.

Kauli hiyo aliitia jana bungeni wakati alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Martha Mlata (CCM).

Mbunge huyo alitaka kujua serikali ina mikakati gani ya kuwawezesha vijana na kuwapatia elimu ili waweze kuzalisha vitunguu kwa wingi kwa kutumia kilimo cha umwagiliaji.

Pia aliitaka serikali ieleze ni mikakati gani ambayo wanaifikiria kuwakopesha vijana ili waweze kununua mashine za kuvuta maji hadi katika mashamba yao kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji kwa lengo la kupata mazao mengi zaidi.

Awali katika swali la msingi Mlata alitaka kujua serikali ina mikakati gani ya kuwasaidia wakulima wa vitunguu ili waweze kulima zao hilo na kuuza zaidi ya mara mbili kwa mwaka.

Katika majibu yake, Malima alisema kuwa serikali inatambua fursa ya kilimo cha vitunguu katika Wilaya mpya ya Mkalama.

Alisema kuwa wizara kwa kushirikiana na Baraza la kuendeleza mazao ya bustani na wadau wengine imeandaa mkakati wa kuendeleza mazao ya bustani ikiwemo zao la vitunguu.

Hata hivyo Malima aliishauri halmashauri ya wilaya hiyo kuanza kuweka kilimo cha vitunguu katika Mipango ya Maendeleo ya kilimo ya Wilaya (DADPs) hususani inayohusu kuweka miundombinu ya umwagiliaji.



juu