HABARI MPYA LA JANA MATANGAZO BEI ZETU WASILIANA NASI TUMA HABARI
jumanne, 10 julai 2012
Yaliyopita
Pekua Tovuti

Jackson Kisambala mkali wa sayansi UMITASHUMTA


na Clescencia Tryphone

 

MWANAFUNZI Jackson Kisambala wa shule ya Msingi Mafinga, mkoani Iringa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ameibuka kinara kwenye fainali ya taaluma ya sayansi, teknolojia na ubunifu kwa kupata alama 34/50 katika mfululizo wa mashindano ya Shule za Msingi, (UMITASHUMTA), mjini hapa.

Kisambala alifuatiwa na Isack James wa Ilboru mkoani Arusha, Kanda ya Kaskazini Magharibi aliyepata alama 30/50 na nafasi ya tatu ikanyakuliwa na Mohamed Omari wa shule ya Petagoni Kanda ya Kati aliyepata alama 30/50 wakati kwa wasichana, Juliana Peter wa shule ya Liwale iliyopo Nyanda za Juu aliibuka kinara akipata alama 33/50.

Nafasi ya pili, ilichukuliwa na Lilian Emanuel wa shule ya Ukombozi aliyepata alama 33/50 na nafasi ya tatu Ikaenda kwa Jesca Raymond wa Himo Kilimanjaro, Kanda ya Kaskazini Mashariki aliyepata alama 32/50.

Katika fainali ya maarifa, Denis Dotto wa shule ya Mtoni Kanda ya Mashariki, aliibuka kinara baada ya kupata alama 44/50 wakati Erick Vincent wa shule ya Miti Mirefu Kanda ya Ziwa alishika nafasi ya pili akipata alama 43/50 na nafasi ya tatu ilichukuliwa na Mussa Almas wa shule ya Town mkoani Tabora, Kanda ya Magharibi aliyepata alama 41/50.

Kwa upande wa wasichana, Nandro Ndimila wa Chunya Nyanda za Juu aliibuka kidedea baada ya kupata alama 44/50 na nafasi ya pili ilichukuliwa na Flomina Agapiti wa Mgulani Dar es Salaam aliyepata alama 42/50 huku Juliana Emily wa shule ya Kakola iliyopo Kanda ya Kaskazini Magharibi akishika nafasi ya tatu kwa alama 42/50.

Kwenye shindano la Hati, Saitoti Opendo wa shule ya Sinya Kanda ya Kaskazin Magharibi aliibuka kidedea kwa alama 49/50 akifuatiwa na Prosper Majan wa Ruaha B ya Kanda ya Mashariki aliyepata alama 47/50 na nafasi ya tatu ilienda kwa Charles Chondi wa Lulindela Kanda ya Magharibi aliyepata alama 42/50.

Upande wa wasichana, Vedisa Likango wa shule ya Mtanda, Kanda ya Kusini aliibuka kinara baada ya kupata alama 48/50 akifuatiwa na Anna Malya wa Shahiri, Kanda ya Kaskazini Mashariki aliyepata alama 46/50 na nafasi ya tatu ilichukuliwa na Elizabeth Shukuru wa Kagera, Kanda ya Magharibi aliyepata alama 45/50.

Kwenye Hisabati, Paulo Paschal wa Kaskazini Mashariki, aliibuka kinara kwa alama 45/50 na nafasi ya pili ilichukuliwa na Ahazi Jared wa Ziwa Magharibi, aliyepata alama 43/50 na Tyson Makoye wa Magharibi akakamata nafasi ya tatu kwa alama 42/50 huku kwa wasichana ni Nuru Ngailo wa Nyanda za Juu akiwa na alama 38/50, Agatha Msula wa Mashariki alama 37/50 na Oliver Mgohele wa Nyanda za Juu Kusini akishika nafasi ya tatu kwa alama 36/50.



juu