HABARI MPYA LA JANA MATANGAZO BEI ZETU WASILIANA NASI TUMA HABARI
jumanne, 10 julai 2012
Yaliyopita
Pekua Tovuti

Mahakama ya Rufaa yaita jalada la ‘Lulu’


na Mwandishi wetu

 

MAHAKAMA ya Rufaa imeitisha jalada la kesi inayomkabili msanii wa maigizo nchini Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu anayetuhumiwa kumuua msanii mwenzake Steven Charles Kanumba baada ya upande wa jamhuri kutaka kufanyiwa marejeo ya umri wake.

Jalada la kesi hiyo liko mahakama kuu tangu Juni 11 mwaka huu baada ya upande wa utetezi kuwasilisha huko kutaka mshtakiwa atambulike kama mkosaji mtoto ambapo shauri hilo liko chini ya Jaji Fauz Twaib.

Jaji Twaib aliiambia mahakama kuwa amepata barua kutoka Mahakama ya Rufaa ikihitaji jalada la kesi hiyo kwa ajili ya kufanya mapitio ambapo walitakiwa kuhakikisha wanawasilisha jalada hilo wiki hii; hata hivyo kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 23.

Juni 30, Lulu kupitia jopo la mawakili watatu, Kenedy Fungamtama, Fulgence Masawe na Peter Kibatala, waliiandikia Mahakama ya Rufaa kuitaka mahakama hiyo kusikiliza mapema shauri hilo la umri.



juu