HABARI MPYA LA JANA MATANGAZO BEI ZETU WASILIANA NASI TUMA HABARI
ijumaa, 14 septemba 2012
Yaliyopita
Pekua Tovuti
Nani kuvikwa taji Miss Kinondoni leo?

Dina Ismail

 

WAREMBO 10 kutoka vitongoji vya Dar Indian Ocean, Ubungo na Sinza, leo wanachuana kumsaka Redd’s Miss Kinondoni 2012, shindano litakalofanyika kwenye ukumbi wa Cassa Complex, Mikocheni, Jijini Dar es Salaam.

Kuelekea shindano hilo, wiki iliyopita warembo hao waliingia kambini katika Hoteli ya JB Belmonte iliyopo katikati ya jiji la Dar es Salaam kujinoa zaidi.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Up and About inayondaa shindano hilo, Vivian Sirikwa anasema safari hii wameazimia kurejesha hadhi na heshima ya Kinondoni katika tasnia hiyo.

Anasema kwa lengo la kufanikia mkakati huo kwa kushiriana na vitongoji husika, waliamua kupata warembo bomba watakaoiwakilisha vema Kanda ya Kinondoni kwenye fainali za Miss Tanzania mwaka huu.

“Tumejipanga vema katika kila idara, yote ni katika kurejesha hadhi ya Kinondoni kwenye fainali za Miss Tanzania,” anasema Vivian.

Vivian anasema, ubora na viwango vya hali ya juu walivyonavyo warembo wa mwaka huu, majaji wa shindano hilo watakuwa na wakati mgumu wa kumchagua mshindi.

Kauli ya Vivian inatokana na umahiri wa Kinondoni kutoa warembo bomba tangu kurejeshwa kwa mashindano ya Miss Tanzania mwaka 1994.

Tangu mwaka huo, Konondoni imeshatwaa taji hilo mara tano Basila Mwanukuzi (1994), Faraja Kotta (2004), Nancy Sumari (2005), Wema Sepetu (2006) na Richa Adhia (2007).

Aidha, Kinondoni imekuwa na historia ya kutoa warembo wanaotikisa katika medani hiyo ndani na nje ya nchi hata kwa wale ambao husindwa kutwaa mataji ya Kanda au Taifa.

Akizungumzia maandalizi, Vivian anasema yamekamilika hivyo wadau wa urembo hawanabudi kujitokeza kwa wingi ukumbi kupata fursa ya kumshuhudia Miss Tanzania mapema.

“Yes, waje kwa wingi ukumbini kumshudia mapema Redd’s Miss Tanzania 2012 mapemaa, nasema hivyo kutokana na kuwaamini warembo wa mwaka huu ni bomba, nina uhakika taji mwaka huu la Miss Tanzania litakuja Kinondoni,” anasisitiza Vivian.

Mkurugenzi huyo anasema pamoja na taji la Miss Kinondoni, leo pia atatangazwa mshindi wa taji la vipaji na lile la Balozi wa Hospitali ya Mwananyamala atayekuwa akifanya kazi za kijamii katika hospitali hiyo kwa mwaka mmoja.

Kuhusu zawadi, Vivian anasema mrembo atakayetwaa taji hilo kutoka kwa Stela Mbuge, ataondoka na seti ya vifaa vya sebuleni ‘Sitting Room Set’ yenye thamani ya sh milioni tano.

“Mshindi wa pili atapata Jokofu la ‘size’ ya familia lenye thamani ya sh milioni tatu, mshindi wa tatu atapata runinga bapa ya inchi 32 yenye thamani ya sh milioni 1.5.

Mshindi wa wanne atapata sh 500,000, mshindi wa tano sh 300, 000 na washiriki waliosalia kila mmoja sh 100,000,”anasema.

Warembo ni Diana Hussein, Kudra Lupatu, Esther Musa, Brigitte Alfred, Jennifer Manu, Judith Sangu, Zulfa Vuai, Mahma Said, Mwantumu Mustafa na Irene David.

Shindano hilo ambalo litapambwa na burudani kutoka bendi ya Skylight, limedhaminiwa na Redd’s Oroginal, JB Belmonte Hotel, Brilliant Mens Boutique, Skylight Entertainment, Kas Freight Limited, Clouds Fm, Magic Fm na Channel 10.



Maoni: 0788 344 566, dinazubeiry@gmail.com au tembelea http://dinaismail.blogspot.com
juu